
Ajali
imetokea usiku huu kati ya treni na basi la Uda linalofanya safari zake
kati ya Kariakoo na Mbagala na kuua mtu mmoja na wengine zaidi ya 45
kujeruhiwa.
Kaimu
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, Ernest Matiku amesema
majeruhi wamepelekwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu.

Hata hivyo, hakuweza kumtaja jina mtu huyo aliyefariki dunia.
“Ni
kweli ajali imetokea kuna kifo cha mtu mmoja na watu wengi wameumia
sana na hivi ninavyozungumza na wewe naelekea Muhimbili,” amesema Kaimu
kamanda huyo.
إرسال تعليق