Joh Makini amshirikisha Falz kwenye ‘Acha Nikupende’

14310693_1609029649390439_1274972269_n
Muziki wa Afrika haujawahi kuunganika kama ulivyo sasa. Akitoka kumshirikisha msanii wa hit ya ‘Omo Alhaji’, Ycee wiki mbili zilizopita, Joh Makini amemshirikisha nyota mwingine wa Nigeria, Falz.
Wawili hao waliopo pamoja kwenye msimu wa nne wa Coke Studio Afrika, walikutana mara ya kwanza Nairobi wiki iliyopita kwenye kurekodi kipindi hicho.
Hata hivyo, wameamua kutoishia hapo. Jumatano, Joh na Falz aliyeshinda tuzo ya BET mwaka huu, waliingia kwenye studio za Wanene Ent. kutayarisha ngoma iitwayo ‘Acha Nikupende.’
“KITU!! #TzNigeriaCollabo It’s a wrap #AchaNikupende feat.@falzthebahdguy beat by @kingluffa #wanenestudios #switchRecords
#GODENGINEERING,” ameandika Joh kwenye Instagram.

Falz alikuwa Tanzania kwenye ziara ya vyombo vya habari.

No comments:

Post a Comment