Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali itakuwa na uwezo na
mamlaka ya kuchunguza watu waliozaliwa na jinsi mbili na kubaini jinsi
tawala yenye nguvu zaidi.

Muswada wa Sheria ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali wa Mwaka 2016, uliopitishwa juzi usiku saa nne bungeni unampa Mkemia Mkuu mamlaka ya kuchunguza na kubaini jinsi ya mtu na kutatua utata kwa mtu atakayekuwa amezaliwa na jinsi mbili.

Muswada wa Sheria ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali wa Mwaka 2016, uliopitishwa juzi usiku saa nne bungeni unampa Mkemia Mkuu mamlaka ya kuchunguza na kubaini jinsi ya mtu na kutatua utata kwa mtu atakayekuwa amezaliwa na jinsi mbili.
“Waheshimiwa wabunge naona wengi wenu mnadhani mkemia mkuu kazi yake
ni kuchunguza vinasaba kubaini uhalali wa mzazi na mtoto, maana naona
wabunge wengi wamelishabikia hilo, lakini katika teknolojia ya vinasaba
yanahusu pia utambuzi wa jinsi, watu unakuta wanawake au wanaume
wanazaliwa jinsi ya kike na kiume, kwa hiyo tunaangalia jinsi tawala ni
ipi ina nguvu,” alisema Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu.
Ummy alikuwa akijibu michango ya wabunge waliochangia wakati wa
kujadili Muswada wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu 2016 kabla ya
kuupitisha juzi usiku, waliotaka mamlaka ya maabara ya mkemia mkuu kutoa
elimu kwa wananchi juu ya shughuli zake.
Alisema kwa sheria hiyo, sasa mkemia mkuu kupitia maabara yake
anaweza kusema jinsi ya kike au ya kiume ndio yenye nguvu, lakini pia
kuna suala la kuhakikisha utambuzi wa mwanadamu hasa wakati yanapotokea
majanga pamoja na watu wanaosafiri kwa makundi.
Alikubaliana na wabunge kuwa iko haja ya kuwaelimisha wananchi juu ya
kazi za maabara ya mkemia mkuu ambao wengi wao wanadhani inafanya kazi
hiyo tu ya kubaini vinasaba vya mzazi na mtoto, lakini sasa wafahamu
hata waliozaliwa na jinsi mbili wanaweza kutegua utata huo kwa kubaini
jinsi tawala au jinsi yenye nguvu zaidi kama ni ya kiume au ya kike
إرسال تعليق