
Hata
hivyo, kwa kura hizo ni hatua ya ushindi wa moja kwa moja kwani ameweza
kuwaacha mbali washiriki wengine wanaowania tuzo hiyo ambayo imekuwa
ikiwaniwa na watu mbalimbali katika Bara la Afrika hasa ambao wameweza
kufanya mambo kwa jamii ikiwemo wafanyabishara wakubwa pamoja na
wanaharakati wa haki za binadamu na Marais wa Nchi wa Bara la Afrika.
Mbali
na Rais Dk. Magufuli wengne wanaowania kinyang’anyiro hicho ni pamoja
na Mwanzilishi wa Capitec Bank, Michiel le Roux, Thuli Madonsela,
Ameenah Gurib na watu wa Rwanda.
Sherehe
maalum za tuzo hiyo zinatarajiwa kufanyika katika Jiji la Nairobi
Nchini Kenya hapo Novemba 17.2016 hivyo endapo Rais Magufuli
atafanikiwa kushinda tuzo hiyo, basi Tanzania itakuwa imepata tuzo hiyo
kwa mara ya pili mfululizo kwani mwaka jana 2015, mshindi wa tuzo hiyo
alikuwa Mkurugenzi Mtendaji na Rais wa Makampuni ya Mohammed Enterprises
Tanzania Limited (MeTL Group), Mohammed Dewji ‘MO’.
Nawe
unaweza kupiga kura yako kwa kuingia kwenye tovuti ya poy2016.com
ambapo baada ya kuingia hapo, unaweza kugusa jina la mtu ambaye
unapendekeza ashinde tuzo na hapo kura itakuwa imehesabiwa (Hii ni kwa
kila kifaa kimoja yaani simu ya mkononi ama kompyuta yako).
Rais
Dk. Magufuli anatimiza mwaka mmoja tokea watanzania wapige kura katika
uchaguzi Mkuu wa Urais 2015, Oktoba 25 na baadae kutangazwa kuwa mshindi
na kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Na Andrew Chale-dewjiblog







إرسال تعليق