Wachina wawili mbaroni kwa kosa la utekaji nyara, Polisi latoa tahadhari kwa wananchi

Kamishna
wa Kanda hiyo, Kamanda Simon Sirro leo amewaambia waandishi wa habari
kuwa, wachina hao walimteka Hong na kumfanyia vitendo vya ukatili ambapo
walitoa masharti ya kupatiwa dola za kimarekani 19,000 ili wamuache
huru.
Kamanda
Sirro amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Wang Young Jing (37) na Chen
Chung Bao (35).Amesema watuhumiwa hao baada ya kufanyiwa upekuzi katika
chumba walichomficha Hong walikuta bomba la sindano, kamba za plastiki
ambavyo vinasadikika kutumika kumjeruhi raia huyo wa china.
Amesema baada ya askari polisi kufanikiwa kumuokoa Hong walimpeleka katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya matibabu.
Aidha,
Kamanda Sirro ametoa taadhari kwa wakazi wa Dar es Salaam kuwa makini
na raia wa kigeni waishio nchini kwa kuwa baadhi yao hushuhulika na
uhalifu ikiwemo utekaji nyara.
Amewataka
wananchi kutoa taarifa pindi watakapobaini kuwa kuna raia wa kigeni
wanaonyanyasa wazawa na kufanya vitendo vya kihalifu
Hisia Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit, sed diam nonummy nibh euismod tincidunt ut laoreet dolore magna aliquam erat volutpat.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Labels
Popular Posts
-
Picha hapo juu zinamwonyesha mwanamke mmoja ambae ni meneja katika taasisi flani ya kifedha,Mwanamke huyo ana tuhumiwa kuwa ...
-
NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA PSLE-2017 EXAMINATION RESULTS ARUSHA DAR ES SALAAM DODOMA IRINGA KAGERA KIGO...
-
SIMULIZI: USILIE NADIA MTUNZI: George Iron Mosenya SMS: 0655 727325 SEHEMU YA KWANZA Mwendo wa kutoka nyumb...

No comments:
Post a Comment