Kipigo cha PSG chamchanganya Luis Enrique

Mchezo wa hatua 16 bora kati ya Paris Saint-German waliokuwa wenyeji wa Barcelona ni wazi umemchanganya kocha wa Barca baada ya dakika 90 kumalizika kwa PSG kuibuka na ushindi wa goli nne kwa bila, kipigo ambacho kinaifanya PSG kuwa timu ya sita kuifunga Barcelona goli nne katika michezo ya Ligi ya Mabigwa Ulaya.
Luis Enrique amesema PSG walijipanga kuwathibiti jambo lililofanya mchezo huo kuwa mgumu kwao tangu dakika ya kwanza hali iliyosababisha kukubali kichapo cha goli nne lakini hatakata tamaa kwani lolote linaweza kutokea katika mchezo wa marudiano.
“Ulikuwa mchezo wenye maafa makubwa, sio ngumu kuelezea, PSG walikuwa wazuri kuliko sisi tangu mwanzo. Walikuwa na kasi na walikuwa wazuri zaidi wakiwa na mpira. Ni wazi tulikuwa dhaifu,
“Ninawajibika kwa hili na hakuna mtu mwingine wa kulaumiwa. Lawama zote zinaniangukia mimi, wachezaji wao hutupa furaha tu na bado kuna hatua nyingine siwezi kupoteza matumaini,” alisema
Magoli ya PSG katika mchezo huo yalifungwa na Angel Di Maria aliyefunga magoli mawili, Julian Draxler na Edinson Cavani, mchezo wa marudiano wa Barcelona na Paris Saint-German utapigwa Machi, 8 katika uwanja wa Camp Nou

Post a Comment

أحدث أقدم