
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania John Pombe Magufuli amemfuta kazi katibu mkuu wa wizara ya
nishati na madini Prof. Justin Ntalikwa.
Rais Magufuli amefanya
hivyo siku chache baada ya kufanya ziara ya kushtukiza bandarini. Hata
hivyo, haijabainika iwapo kuna uhusiano kati ya ziara hiyo na kufutwa
kwake Ntalikwa.Rais Magufuli alifanya ziara hiyo kwa lengo la kufuatilia utekelezaji wa maelekezo aliyoyatoa kwa nyakati tofauti, juu ya kudhibiti udanganyifu wa mizigo inayoingia na kutoka nchini kupitia bandari hiyo, ikiwemo usafirishaji wa mchanga wa madini kwenda nje ya nchi.
Katika ziara hiyo Rais Magufuli alishuhudia makontena 20 ya mchanga wenye madini kutoka kwenye migodi iliyopo kanda ya ziwa, ambayo yamezuiliwa kusafirishwa nje ya nchi tangu alipotoa agizo la kupiga marufuku usafirishaji wa mchanga nje ya nchi tarehe 2 Machi, 2017

Post a Comment