Rais wa Jamhuri ya Muungano wa 
Tanzania John Pombe Magufuli amemfuta kazi katibu mkuu wa wizara ya 
nishati na madini Prof. Justin Ntalikwa.
Rais Magufuli amefanya 
hivyo siku chache baada ya kufanya ziara ya kushtukiza bandarini. Hata 
hivyo, haijabainika iwapo kuna uhusiano kati ya ziara hiyo na kufutwa 
kwake Ntalikwa.Rais Magufuli alifanya ziara hiyo kwa lengo la kufuatilia utekelezaji wa maelekezo aliyoyatoa kwa nyakati tofauti, juu ya kudhibiti udanganyifu wa mizigo inayoingia na kutoka nchini kupitia bandari hiyo, ikiwemo usafirishaji wa mchanga wa madini kwenda nje ya nchi.
Katika ziara hiyo Rais Magufuli alishuhudia makontena 20 ya mchanga wenye madini kutoka kwenye migodi iliyopo kanda ya ziwa, ambayo yamezuiliwa kusafirishwa nje ya nchi tangu alipotoa agizo la kupiga marufuku usafirishaji wa mchanga nje ya nchi tarehe 2 Machi, 2017
 Pamoja na kushuhudia makontena hayo, Rais Magufuli alimuagiza mkuu wa 
Jeshi la Polisi Nchini IGP - Ernest Mangu na vyombo vingine vya dola, 
kuhakikisha mchanga wa madini unashikiliwa popote ulipo, mpaka hapo 
uchunguzi wa kina utakapofanyika kubaini ukweli.Akiwa bandarini hapo Rais Magufuli pia, alishuhudia udanganyifu mwingine
 unaofanywa na wafanyabiashara wanaoagiza mizigo kutoka nje, ya nchi 
baada ya kuoneshwa makontena ambayo nyaraka zinaonyesha yamebeba mitumba
 ya nguo na viatu, wakati ndani yake kila kontena moja limebeba magari 
matatu ya kifahari.

إرسال تعليق