Watu kadha wapigwa risasi kwenye klabu nchini Marekani

Watu kadha wapigwa risasi kwenye klabu nchini Marekani 
Mtu mmoja ameuawa na wengine 14 kujeruhiwa kufuatia ufyatuaji wa risasi kwenye klabu ya usiku huko Cincinati jimbo la Ohio.
Takriban watu wawili waliokuwa na silaha walitekeleza shambulizi kwa mujibu wa polisi.
Watu kadha walipata majeraha mabaya.
"Tuko kati kati ya hali mbaya alisema mkuu wa polisi" Paul Neudigate.
Kapteni wa polisi Kimberly Williams alisema kuwa polisi hawana taraifa kuhusu washambuliaji hao.
Hadi wakati huu kile kilochosababisha kutokea ufyatuaji huo bado hakijulikani.
Ufyatuaji huo ulitokea saa 05:00 GMT wakati mamia ya wtu walikuwa eneo hilo.
Kisa hicho kinatokea chini ya mwaka baada ya Omar Mateen, kufyatua risasi kwenye klabu ya wapenzi wa jinsia moja mjini Orlando huko Florida.
Mateen aliwaua watu 49 katika kisa ya kibaya zaidi cha ufyatuaji risasi katika historia ya Marekani.

Post a Comment

أحدث أقدم