Wakati
Chama cha Demokrasia na Maendeleo, kikisisitiza uchunguzi wa
kushambuliwa Mbunge Tundu Lissu ufanywe na vyombo vya kimataifa familia
yake imezungumza kuhusiana na tukio hilo na kusema wao hawana mashaka
na jeshi la polisi kufanya uchunguzi.
Kauli
hiyo ya familia imetolewa Jijini Arusha na Wakili Alute Mughwai ambaye
ni kaka wa Tundu Lissu ambapo amesema mpaka sasa familia haijatoa
maamuzi ya moja kwa moja ni nani achunguze tukio hilo lakini mpaka sasa
wana imani na uchunguzi unaofanywa na jeshi la polisi.
Wakili
Mughwai amesema pindi familia ikikaa kwa mara nyingine watazungumzia
suala hilo na kuja na kauli nyingine ya pamoja ya familia kuhusiana na
msimamo wao wa ni nani afanye uchunguzi wa tukio hilo kama kutakua na
ulazima wa kufanya hivyo.
"Hatujakaa
sisi kama wanafamilia kutoa msimamo wetu kuhusiana na uchunguzi wa
tukio hilo, kwamba hatuna imani na jeshi la polisi na uchunguzi ufanywe
na vyombo vya kimataifa lakini kama tukikutana tukawa na msimamo wetu
tutatoa maoni yetu kama haja itakuwepo," amesema Mughwai.
Aidha
ameongeza kwamba wao kama familia hawana tatizo lolote la kibiashara,
wala hawana tatizo na Tundu Lissu hivyo watu wasije wakaunganisha
matukio na kuhusisha kushambuliwa kwake na matukio ya biashara na
kuongeza kuwa ndugu yao siyo mfanyabiashara bali biashara yake ni siasa
pamoja sheria.
Mbali
na hayo amewataka jeshi la polisi kuanzia uchunguzi wao kwa kufuatilia
mkutano aliokuwa akizungumzia suala la Bombadier kukwama nchini Canada
na alipozungumzia suala la kufuatiliwa na watu asiowafahamu.
Hata
hivyo Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema jana kilisema
kinahitaji serikali iruhusu wachunguzi wa kimataifa kuingia nchini
kufanya uchunguzi juu ya shambulio la kupigwa risasi kwa Mbunge na
Mwanasheria wao Tundu Lissu mnamo Septemba 7 mwaka huu mchana eneo la
'Area D' mjini Dodoma
Post a Comment