Spika
Ndugai ametoa kauli hiyo Bungeni ambapo amesema Zitto Kabwe hawezi na
hapaswi kujibizana naye, na kumtaka Zitto Kabwe kutomfananisha na
aliyekuwa Spika wa Bunge marehemu Samuel Sitta, kwani hawezi kufanana
naye na kila mtu ana muda wake, kama ambavyo Spika wa bunge aliyepita
mama Anna Makinda alivyokuwa na muda wake kuliongoza bunge hilo.
"Hawa
ni watu nawaheshimu sana na wamenilea sana na ni sehemu nilipofika
hapa leo. Utanilinganishaje mimi na milima mikubwa kama Kilimanjaro?
Hata siku moja sikio haliwezi kuzidi sikio," amesema.
Amesema katika Bunge la 9 Zitto aliwahi kupeleka hoja ya Mgodi wa Buzwagi ambayo ilikataliwa na Bunge lakini ikazuka hoja ya kimaadili ambapo alihukumiwa hapo hapo.
"Alihukumiwa hapo hapo akapigwa miezi mitatu. Mnataka niende mkuku mkuku kama lile la Bunge la tisa nifanane na mzee Sitta? Hilo pia naliweza kwa nini mnaalika matatizo nashangaa unapambana na Spika," amesema.
"Ninauwezo wa kupiga marufuku kuzungumza hadi miaka yote mitano iishe hauna pa kwenda, hakuna cha swali, nyongeza wala kuzungumza utanifanya nini?
Amemtaka kupambana na mtu mwingine lakini sio yeye.
"Kwa haya ya Spika sina sababu nayo lakini ya kulidharau Bunge hayo sitaweza kuyavumilia nitalinda mihimili huu kwa nguvu zangu zote," amesema.
Amesema hawawezi kuacha wabunge kulidhalilisha Bunge na kuhoji kwamba watachukuliaje Watanzania wengine watakapolidhalilisha Bunge.
Amesema hilo kosa la pili kwa Zitto na kuagiza liende katika kamati ya maadili.
"Tutaenda sambamba mguu kwa mguu hadi kieleweke," amesema

Hapo
jana Spika Ndugai alimtaka Zitto Kabwe kufika kwenye kamati ya maadili
kutoa maelezo juu ya taarifa alizoziweka kwenye mtandao, na Zitto Kabwe
kumjibu kuwa mambo anayoyafanya Spika yanaporomosha bunge
Post a Comment