ITALIA ikiwa na kinara Mario Balotelli, jana ilifanikiwa kutinga hatua
ya nusu fainali ya michuano ya Kombe la Euro 2012 baada ya kuitandika
England yenye kinara Wayne Rooney kwa penalti 4-2.
Mchezo huo ulianza kwa kasi huku timu zote mbili zikishambulia kwa nguvu na ndani ya dakika kumi kila timu ilishafika langoni kwa mpinzani wake.
Mshambuliaji Mario Balotelli alikosa mabao mawili akiwa anatazamana yeye na kipa wa England, Joe Hart, lakini pia England ilipoteza nafasi nzuri baada ya Glen Johnson kuupiga mpira ambao uliokolewa kiufundi na kipa wa Italia, Gianluigi Buffon.
Italia ambayo ilikuwa inapewa nafasi kubwa ya kutinga hatua ya nusu fainali ilipata nafasi nyingi sana za kufunga ndani ya dakika 120, lakini washambuliaji wake hawakuwa makini kuuweka mpira kimiani.
Hata hivyo kipa wa Italia, Buffon ndiye alikuwa shujaa kwenye mchezo huo baada ya kufanikiwa kuokoa mkwaju wa Ashley Cole huku shuti la Ashley Young akigongesha mwamba.
Wachezaji waliofunga penalti za England ni Steven Gerrard na Wayne Rooney waliofunga kwa Italia ni Balotelli, Andrea Pirlo, Antonio Nocerino na Alessandro Diamanti.
Sasa Italia itavaana na Ujerumani

Post a Comment