WAKATI mgomo wa madaktari umesitishwa na Serikali, Chama cha Walimu
Tanzania (CWT), kimesema maandalizi ya mgomo wao yanaendelea iwapo
Serikali haitatekeleza makubaliano yao watafanya mgomo usio na mwisho
kuanzia Julai 16, mwaka huu.
Mgomo huo utaanza kama Tume ya Usuluhishi na Upatanishi (CMA) haitatoa uamuzi wa kuridhisha utakaotolewa Juni 26, mwaka huu.
CWT
kilisema iwapo hakitaridhishwa na uamuzi huo, walimu nchi nzima
watapiga kura za siri kuhusiana na matokeo hayo, kisha kutoa notisi ya
saa 48 kabla ya kuanza mgomo.
Pia, kilisema hakijatangaza mgomo
bali kilichopo ni mgogoro ambao kama Serikali itashindwa kutekeza
mapendekezo na makubaliano waliyotoa, wanaweza kupelekea kufikia mgomo
nchi nzima.
Akizungumza kwenye mjadala wa kiashirio cha ajira
ulioshirikisha viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania
(Tucta) na Chama cha Waajiri Tanzania (Ate), Mkuu wa Idara ya Utetezi
Walimu na Mwanasheria wa CWT, Leonard Haule, alisema hivi sasa
imetangaza mgogoro na Serikali.
Haule alisema mgogoro huo unatoa
fursa ya majadiliano au utekelezaji madai yao, iwapo mwafaka hautafikiwa
Julai 16, wataanza rasmi mgomo nchini nzima.
“Sisi hatujatangaza
mgomo wa walimu, bali tumetangaza mgogoro ambao kama mambo tuliyoyataka
hayatatekelezwa, basi unaweza kupelekea mgomo,” alisema Haule.
Alisema
Juni 5, mwaka huu mkoani Dodoma, CWT ilipitisha azimio la kutangaza
mgogoro kwa lengo la kutaka Serikali kutekeleza yale waliyokubaliana
kuhusu nyongeza za mishahara, posho za kufundishia na posho kwa walimu
wanaofundisha katika mazingira magumu.
Alitaja madai yao kuwa, ni
nyongeza ya mshahara kwa asilimia 100, posho ya ufundishaji ambayo kwa
walimu wa sayansi wanataka walipwe asilimia 55 ya mshahara wao kila
mwisho wa mwezi na asilimia 50 kwa walimu wa masomo mengine.
Mengine ni posho ya mazingira magumu yanayotambuliwa na Serikali kwa walimu, ambayo ni asilimia 30 ya mshahara kwa kila mwalimu
Post a Comment