Mgomo wa madaktari waendelea kimya kimya

Mgomo wa madaktari waendelea kimya kimya

WAGONJWA katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC, mjini Moshi wameanza kuonja shubiri ya mgomo, baada ya madaktari zaidi ya 80 wa hospitali hiyo, kuanza rasmi mgomo usiokuwa na kikomo.

Habari zinadai kuwa hatua ya madaktari walioko kwenye majaribio na wale wanaosomea udaktari bingwa, inatokana na vikao vyao vilivyofanyika jana asubuhi.

“Intern Doctors ndio wameweka vifaa vyao chini na wameondoka wote na hawako wodini,hawa wako kati ya 70 na 80 hivi hali sio nzuri hata kidogo,”alidokeza daktari mmoja bingwa katika hospitali hiyo.

Hospitali ya KCMC ina aina mbili za madaktari ambao ni wale walioajiriwa na Serikali na wale walioajiriwa na Shirika la kidini la Msamaria Mwema (GSF) na waliogoma ni wale wa Serikali.

Kwa mujibu wa daktari huyo, madaktari hao tayari wameshamaliza mafunzo yao ya udaktari lakini kwa sasa wako, katika majaribio kwa vitendo.Habari zilisema madaktari wanaosomea ubingwa walikuwa katika maandalizi ya mwisho ya kuanza mgomo na baadhi yao hawakuwa wakitoa huduma, jambo lilioashiria kuwapo kwa mgomo baridi.

Taarifa zilizopatikana baadaye jana alasiri zilisema madaktari waliokuwa wakitoa huduma ni wale mabingwa na kwamba haijulikani wengine walikuwa wapi.Muuguzi mmoja katika wodi ya wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu, aliliambia gazeti hili kuwa huduma zilikuwa zinatolewa na madaktari bingwa tu na wale ambao ajira zao ziko shirika la GSF, ambao kwa Idadi ni wachache.

Mkazi mmoja wa Moshi, Raymond Mushi alisema kaka yake ambaye anasumbuliwa na kuziba kwa kibofu cha mkojo, alitakiwa kufanyiwa upasuaji jana, lakini kwa sababu ya mgomo aliruhusiwa kurudi nyumbani.
Mkurugenzi Mwendeshaji wa Hospitali ya KCMC, Dk. Moshi Ntabaye, hakupatikana kuzungumzia habari hizi kwa sababu simu yake, ilikuwa haipokelewi na ilielezwa kuwa alikuwa katika vikao vya kunusuru mgomo.


Taarifa kutoka Hospitali ya Mkoa wa Kilimanjaro ya Mawenzi na hospitali za Wilaya za Same,Mwanga na Hai zilisema huduma za matababu zilikuwa zikiendelea kama kawaida.


Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro, Leonidas Gama, alisema hakuwa na taarifa za kuanza kwa mgomo kwa kuwa alikuwa bungeni mjini Dodoma na kuahidi kufuatilia suala hilo kwa ukaribu.
Habari kutoka Mbeya zilisema wagonjwa katika Hospitali ya Rufaa  Mbeya na  ile ya Kitengo cha Wazazi ya Meta, jana waliendelea kusotea huduma kufuatia mgomo unaoendelea.

Wakizungumza na mwandishi wa habari hiyi katika huko Meta, baadhi ya wajawazito walisema  wanaendelea kusotea matibabu kufuatia mgomo wa madaktari.

"Tumekaa tu hapa tangu saa 1:00 asubuhi,hakuna mganga  anayejali na manesi waliopo hapa wanatushauri tuondoke tu,”alisema Mariam Christopher.


Muuguzi mmoja ambaye hakutaka jina lake litajwe alikiri kuwa hali ni mbaya na kwamba hiyo inatokana na mgomo wa madaktari.

Mganga Mkuu wa Hospiatali ya Mkoa wa Mbeya, Dk. Seif Mhina, alikiri kuwapokea wanawake wengi  wajawazito wakitokea Hospiatali ya wazazi  ya Meta.

Alisema hata hivyo hospitali hiyo sasa imezidiwa na wagonjwa wanaotoka katika hospitali mbalimbali.

“Nikweli  tunapokea wagonjwa wengi ambao ni akina wajawazito wakitokea Meta,hali  sasa inaelekea kuwa mbaya sana hapa kwetu kwani miundombinu katika wodi ya akina mama  wajawazito haitoshi," alisema Dk Mhina.

Mkurugenzi wa hospitali hiyo Dk Eliuter Samky hakupatikana kutokana na kile kilichoezwa kuwa alikuwa na kikao cha dharura kilichoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro.

Habari kutoka Mwanza  zilisema hali katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando bado ni tete.

Akizungumza na Mwananchi,  mmoja wa madaktari waliogoma  Dk Geogre Andrian alisema hawapo tayari kurudi kazini hadi hapo Serikali itakapotekeleza madai yao.

“Huu ni wakati wa ukweli na uwazi kama Serikali imetekeleza nusu ya madai yetu kwani nini hawajaelezea wazi yale ambayo wameyafanya ili watanzania wote waweze kushuhudia utekelezwaji wa madai hayo,”alihoji Dk Adriano.

Aliendelea kwa kusema kuwa madakrati waliopo katika mgomo ni madkataria mabao ni wazalendo na kudai kuwe wengi wa madaktari wemekimbilia nchi za nje kwa sababu huko wanapata maslahi mazuri.

Akitolea mfano wa nchini Rwanda alisema kuwa madaktari huko wanalipwa kiasi cha dola 15000 na kusema kuwa hiyo ni moja ya nchi katika afrika masharikia mabayo inawajali madaktari wake.

Jijini Dar es Salaam, habari zilisema
madaktari wanaofanya kazi katika Taasisi ya Mifupa ya Muhimbili ni  wakuu wa idara na vitengo.
Mmoja wa maaofisa katika hospitali hiyo, alisema mgomo unaendelea, umeathiri utoaji wa huduma katika Hospitali ya Muhimbili.
Chanzo:- Mwananchi

Post a Comment

أحدث أقدم