Makunga kusomewa maelezo ya awali leo

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, leo inatarajiwa kumsomea maelezo ya awali Mhariri Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Mwananchi Communications Ltd (MCL) Theophil Makunga katika kesi inayomkabili.Maelezo hayo yatasomwa baada ya kushindwa kusomwa kutokana na uzuru uliotolewa Mei 15 mwaka huu na mshtakiwa wa pili katika kesi hiyo, Absalom Kibanda.

Kibanda na Makunga wanakabiliwa na shtaka la kuandika na kuchapisha makala ya uchochezi kama mshtakiwa wa pili na wa tatu. Mshtakiwa wa kwanza katika kesi hiyo ni mwandishi wa makala hiyo, Samsoni Mwigamba.

Makunga aliunganishwa katika kesi hiyo kutokana na mtambo wa uchapaji wa kampuni ya MCL inayochapisha magazeti ya Mwananchi, The Citizen na Mwanaspoti kuchapisha gazeti la Tanzania Daima likiwa na makala inayodaiwa kuwahamasisha askari kugoma kutii amri za viongozi wao wakati yeye alipokuwa akikaimu nafasi ya Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo.

Anadaiwa kutenda kosa hilo wakati akikaimu nafasi ya Mkurugenzi Mtendaji wa kamapuni hiyo, baada ya Mkurugenzi aliyekuwepo, Sam Sholei kumaliza muda wake, nafasi ambayo kwa saa inashikiliwa na Tido Mhando.

Mwigamba ni mshtakiwa wa kwanza kwa kuwa kuwa ndiye mwandishi wa makala hayo na Kibanda ndiye Mhariri Mtendaji wa gazeti hilo anayedaiwa kuruhushu makala hayo yachapishwe katika gazeti lake.

Kesi hiyo iliiitwa mahakamani hapo Mei 15 kwa ajili ya usikilizwaji wa awali, ambapo washtakiwa walitakiwa kusomewa maelezo ya awali ya kesi hiyo, lakini ilikwama, kutokana na Kibanda kuutaarifu upande wa mashtaka kuwa asikuwepo mahakamani siku hiyo

Post a Comment

أحدث أقدم