MWANA FA, OMMY DIMPOZ KUPIGA KAZI USIKU WA MTU MZIMA DAWA

MWANA FA, OMMY DIMPOZ KUPIGA KAZI USIKU WA MTU MZIMA DAWA

 
WAKALI wa muziki wa kizazi kipya Mwana FA na Ommy Dimpoz wanatarajiwa kumsindikiza chipukizi mkongwe kwenye muziki wa kizazi kipya Bi Kidude kwenye maonyesho yake matatu Mkoani Mwanza. Maonyesho hayo yatafanyika kuanzia Julai sita, saba na nane, katika kumbi mbalimbali mkoani Mwanza.

Ziara hiyo imepewa jina la usiku wa mtu mzima dawa likiandaliwa na Meneja wa TMK Family, Said Fella. Fella aliliambia Blog hii kuwaonyesho la kwanza litafanyika Julai 6 (Ijumaa) katika Ukumbi wa Villa Park, jijini Mwanza.

Maonyesho mengine yatafanyika Julai 7 (Jumamosi) kwenye Ukumbi wa Ambassador Club uliyopo Geita na lile onyesho la mwisho litakuwa Jumapili ya Julai 8 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza.

Wasanii wengine watakaokuwemo kwenye ziara hiyo ya mtu mzima dawa, itakuwa wakali wote kutoka TMK Family kama Temba, Chegge na Aslay.

Post a Comment

أحدث أقدم