RONALDO AIPELEKA URENO NUSU FAINALI

RONALDO AIPELEKA URENO NUSU FAINALI



Cristiano Ronaldo scores
BAO pekee la Cristiano Ronaldo dhidi ya jamhuri ya Czech usiku huu, limeiwezesha Ureno kutinga Nusu Fainali ya Euro 2012.
Ronaldo, ambaye alifunga mabao mawili dhidi ya Uholanzi, aling'ara sana kwenye mchezo wa leo kipindi cha kwanza hadi cha pili.
Lakini ilimbidi asubiri hadi zikiwa zimesalia dakika 12 mchezo kumalizika ili kufunga bao hilo muhimu, akimtungua mmoja wa makipa bora duniani kwa sasa, Petr Cech.
Ureno sasa itamenyana na mshindi kati ya Hispania au Ufaransa katika Nusu Fainali.

Post a Comment

Previous Post Next Post