BILIONEA mmoja anayemiliki kiasi kikubwa katika hisa za klabu ya Arsenal, Alisher Usmanov anasema angependa kununua hisa zaidi za klabu hio ingawa hana nia ya kupata nafasi kwenye bodi inayoongoza klabu.
Usmanov ambaye ndiye tajiri mwenye vipesa kuliko tajiri mwingine nchini
jimbo la zamani la Urussi la Uzbekistan, ni mmoja wa matajiri kadhaa
wanaomiliki hisa katika klabu za Uingereza kama Roman Abramovich huko
Chelsea na Anton Zingarevich wa Reading.
Usmanov ameliambia shirika la habari la Reuters nje ya mji wa Petersburg
kua 'daima na kwa kiwango chochote, nipo tayari kuongezea kiwango cha
hisa zangu.
Usmanov, ambaye utajiri wake umetokana na biashara ya chuma na
teknolojia anaweza kujijengea umaarufu na nafasi kwenye bodi kutokana na
kiwango cha hisa atakazowekeza.
Chombo cha Red and White, kinachomilikiwa na Usmanov kwa ushirikiano na
Farhad Moshiri,wana miliki asili mia 29.72 ya hisa katika Arsenal,kwa
mujibu wa Tovuti ya klabu hio.
Licha ya uwezo huo, Usmanov hajioni akiwa kwenye bodi ya viongozi wa
Arsenal, na kwa kauli yake anasema 'singependa kuhudhuria mkutano wa
bodi bila kualikwa.
Kwa mujibu wa habari za vyombo vya habari mmiliki mkubwa wa hisa za
Arsenal, Kroenke anachukizwa kusikia kama Usmanov angepewa nafasi kwenye
bodi ya Arsenal.
Post a Comment