DAKTARI AKAMATWA AKIMBAKA MSICHANA ALIYEKUWA AKIMFANYIA ABOSHENI.

Daktari mmoja ambaye pia ni mwanafunzi wa chuo cha udaktari nchini Ghana anashikiliwa na polisi kwa kosa la kumlazimisha msichana mmoja nchini humo kufanya naye mapenzi wakati alipoenda ofisini kwake kwa lengo la kutoa ujauzito. Daktari huyo anayefanya kazi kwenye hospitali moja iliyopo Madina mjini Acra Ghana alikutwa na kosa hilo baada ya Anas Aremeyaw (mwandishi wa habari) kutega kamera kwenye chumba cha kufanyia kazi hiyo baada ya kupata taarifa ya kuwepo kwa
vitendo hivyo viovu kutoka kwa daktari huyo ambapo ndipo aliponaswa na kamera hiyo akilazimisha ngono kutoka kwa mteja wake aliyefika siku hiyo kwa ajili ya huduma hiyo na daktari alipata hamasa ya kutaka ngono baada ya mteja wake kutoa nguo zake. 
Daktari huyo alimtishia mteja wake kuwa hatatoa ujauzito huo kama hatakubali kufanya naye ngono.Inasemekana kuwa daktari huyo ameshatembea na wanawake zaidi ya 52 kwa nyakati tofauti kwa kutumia njia yake hiyo ambao wengi wao wana umri kati ya miaka 20-40.

Post a Comment

أحدث أقدم