Football | World Cup 2014
BEKI
wa kimataifa wa Denmark mwenye asili ya Tanzania, Patrick Mtiliga
amesema kwamba aligoma kuingia akitokea benchi kwenye mechi ya kuwania
tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia dhidi ya Italia, kwa sababu
hakufurahia kuanzishiwa benchi kwenye mchezo huo.
Kocha
Morten Olsen alisema juzi kwamba alishangazwa mno na beki huyo mwenye
umri wa miaka 31 kukataa kupasha ili aingie kucheza akitokea benchi.
Amesema katika maisha yake yote ya kuwa kocha wa timu ya taifa, Mtiliga hatacheazea tena Denmark.
"Nilisikitishwa mno na nilifikiri ni kudharauliwa," alisema Mtiliga baada ya mazoezi leo.
"Ningemudu
hilo vizuri na kwa mawasiliano mazuri," alisema beki huyo anayechezea
klabu bingwa Denmark, FC Nordsjaelland. Wenyeji Italia walishinda 3-1
Jumanne.
إرسال تعليق