Mrisho Ngassa; Nipeni muda muone mambo ya hatari |
Na Mahmoud Zubeiry
KIUNGO
Mrisho Khalfan Ngassa, amesema kwamba bado anaizoea taratibu staili ya
uchezaji ya timu yake mpya, Simba SC na nafasi mpya anayopangwa kwa sasa
na anaamini hadi Januari mwakani atakuwa ameizoea na kufanya ‘mambo ya
hatari’.
Akizungumza na BIN ZUBEIRY jana,
Ngassa alisema kwamba Simba wanacheza mfumo tofauti na ambao ulikuwa
unatumiwa na timu yake ya zamani, Azam FC hivyo anaendelea kujifunza na
kuizoea.
“Mchezaji
unapoingia timu mpya, kawaida unakutana na mambo mengi mapya, inabidi
sana ujifunze na kuzoea. Unacheza na watu wapya, ambao inabidi ujifunze
namna ya kucheza nao na kuzoeana nao,”alisema Ngassa.
Ngassa
alisema angalau anekutana na wachezaji ambao anacheza nao timu ya
taifa, lakini safu ya ushambuliaji ya Simba inaundwa na wachezaji wengi
wa kigeni kama Emmanuel Okwi, Daniel Akuffo na Felix Sunzu.
“Inabidi
sana nijifunze taratibu, hata hivyo najisifu kwamba naendelea vizuri na
hadi kufika Januari hivi, nitakuwa nimekwishazoea na kufanya mambo ya
hatari,”alisema Ngassa na kusistiza hajashuka kiwango, ni mazingira
mapya tu.
Ngassa
juzi alifunga bao lake la tatu tangu ajiunge na Simba Agosti mwaka huu,
akitokea Azam FC wakati Simba ikilazimishwa sare ya kufungana mabao 2-2
na Kagera kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, hiyo ikiwa sare ya
pili mfululizo kwa Wekundu hao wa Msimbazi, baada ya Jumamosi pia
kulazimishwa sare ya bila kufungana na Coastal Union mjini Tanga.
Kwa
matokeo hayo, Simba imefikisha pointi 18 na kuendelea kuongoza Ligi
Kuu, kutokana na Azam FC kulazimishwa sare ya bila kufungana na Prisons
kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
Hadi
mapumziko, Simba SC walikuwa mbele kwa bao 1-0, lililotiwa kimiani na
mshambuliaji wa kimataifa wa Zambia, Felix Mumba Sunzu Jr. dakika ya
nane, akiunganisha kwa kichwa krosi ya Nassor Masoud ‘Chollo’ kutoka
wingi ya kulia.
Kwa
ujumla kipindi cha kwanza timu zote zilishambuliana kwa zamu, ingawa ni
Simba walioonekana kufanya mashambulizi ‘yenye akili’ zaidi.
Kipindi
cha pili Simba ilirudi na moto tena na katika dakika ya 51, Mrisho
Khalfan Ngassa aliifungia timu hiyo bao la pili kwa shuti kali
lililowababatiza mabeki wa timu hiyo na kutinga nyavuni.
Baada
ya hapo, Kagera walizinduka na kuanza kulishambulia lango la Simba
kupitia pembeni na katika dakika ya 64 Themi Felix aliunganisha kwa
kichwa krosi ya George Kavilla na kuifungia Kagera bao la kwanza.
Bao
liliwazindua Kagera, ambao waliongeza kasi ya kulishambulia lango la
Simba na katika dakika ya 66, Juma Nyosso alimkwatua kwenye eneo la
hatari Paul Ngwai na Salum Kanoni akaenda kumtungua Juma Kaseja,
akiisawazishia Kagera.
Baada ya hapo timu zilianza kushambuliana kwa zamu na mpira ulinoga zaidi kutokana na mashambulizi ya pande zote mbili.
Chanzo:- http://bongostaz.blogspot.com/
إرسال تعليق