"HUWEZI KUNIPATA BILA KUWA NA MILIONI MOJA:......JACK WOLPER


WAKATI filamu nyingi za bongo bajeti yake si ile ya kushtua mtu kama kazi za wasanii wa mbele, na kwa kulitazama hilo msanii Jackline Wolper ameamua kuweka wazi fungu lake ili kwa wale wanaotaka kumshirikisha kwenye filamu zao basi wajue kuwa anaweza kucheza kuanzia milioni 1 na kuendelea chini ya hapo hapotezi muda.

Wasanii wa Tanzania wanatatizo kubwa la kutotumia pesa ya kutosha katika utengenezaji wa filamu zao, na wengi bajeti zao ni chini ya mil 8, hivyo kwa kiasi anachokitaka Wolper sijui kama ni kweli anaweza kulipwa ingawa wengi tumewazoea wakisema hivyo lakini mwisho wa siku unasikia kacheza filamu kwa laki 2.


Msanii huyo aliweka wazi ishu hiyo wakati akizungumza kwenye mahojiano na televisheni ya
Clouds TV kupitia kipindi cha Take One, ambapo aliulizwa kiasi anachotaka kulipwa kucheza filamu, ndipo alipotaja fungu hilo.

“Kwa kweli suala la kulipwa mara nyingi huwa inatengemea na filamu yenyewe lakini kwa upande wangu naweza kusema kwamba kuanzia milioni 1 hapo nafanya kazi,”
alisema.

Post a Comment

أحدث أقدم