Sultan Qaboos bin Said Al Said akimpongeza Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete baada ya kumtunuku nishani ya juu ya heshima
ya Taifa la Oman jana jioni katika kasri ya AL Alam. Jijini Muscat Oman
jana jioni .Rais Kikwete aliwasili nchini Oman jana jioni kwa ziara
rasmi ya siku nne.
Sultani wa Oman,Qaboos bin Said Al Said akimtunuku Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete nishani ya juu ya heshima, Taifa la Oman
wakati wa dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa kwa heshima ya Rais Kikwete na
ujumbe wake jana jioni katika kasri ya AL Alam jijini Muscat Oman.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpa zawadi mwenyeji
wake Sultani wa Oman Qaboos bin Said Al Said katika kasri ya AL Alam
jijini Muscat Oman jana jioni muda mfupi kabla ya dhifa ya kitaifa
aliyoandaliwa kwa heshima yake.Picha na Freddy Maro-IKULU
إرسال تعليق