MTAZAME ‘DOGO’ ATAKAYEWARITHI MAJERUHI MARCELO, FABIO COENTRAO KATIKA KIKOSI CHA REAL MADRID… ANAITWA JORGE CASADAO WA KIKOSI CHA VIJANA REAL

Jorge Casadao: Siogopi kitu... niko tayari kuziba nafasi za Marcelo, Coentrao... !

Jorge akiwa na wenzake wa Real Madrid Castilla
Beki wa kushoto wa timu ya vijana ya Real Madrid a.k.a ‘Castilla’,  Jorge Casadao, amesema kuwa yuko tayari kuwamo katika kikosi cha kwanza kuziba nafasi za nyota wao Marcelo na Fabio Coentrao wanaosumbuliwa na majeraha.

Casado anajiandaa kutwaa nafasi hiyo baada ya Marcelo kuvunjika mguu na hivyo kuwa nje ya uwanja kwa miezi mitatu na Fabio Coentrao ni majeruhi pia na atakuwa nje kwa mwezi mmoja.

"Hakuna yeyote anayefurahia kuumia. Wanaweza kufungua milango zaidi kwa wengine ila mimi sina haraka. Niko tayari, lakini Castilla (kikosi cha vijana) ndiyo timu yangu," amesema Casado.

Post a Comment

أحدث أقدم