Wajumbe
wa Baraza la Wawakilishi waliotoa maoni yao yao mbele ya Tume ya
Mabadiliko ya Katiba wametaka Zanzibar na Tanganyika ziwe na Mamlaka
kamili huku mfumo wa muundo wa Muungano ukiwa wa mkataba…
Mwakilishi
wa Jimbo la Mji Mkongwe,Ismail Jussa Ladhu alisema kwa mfumo wa muundo
wa Muungano uliopo kamwe matatizo ya Muungano hayatasita hivyo ni lazima
kubadili na kuwa na muundo wa mkataba ambao utakuwa ndio suluhisho la
kero za Muungano.
“Kwa
mfumo huu tuliokuwa nao, idadi ya Serikali haziwezi kutatua kero
,katika matatizo haya sioni njia nyengine zaidi ya Muungano wa mkataba”
Alisema Jussa.
Katika
utangulizi wake,Jussa alisema tangu siku ya kwanza ya kuasisiwa kwa
Muungano huu kulianza matatizo akitoa mfano kuwa wataalam waliotumika
kuandaa hati za Muungano hawakuwa Watanganyika wala Wazanzibari, ni
raia wa Uingereza walioegemea zaidi kwenye mazingira ya nchi yao.
Mwakilishi
wa Jimbo la Mwanakwerekwe(CCM),Shamsi Vuai Nahodha alipendekeza kuwepo
na mabunge matatu chini ya mfumo wa muundo wa Muungano wa Serikali
mbili, liwepo Baraza la Wawakilishi kwa ajili ya Zanzibar, Bunge la
Jamhuri ya Muungano la wote na liwepo Bunge dogo kwa ajili ya
Tanganyika tu kwa mambo yasiyokuwa ya Muungano.
Shamsi
ambaye pia ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa alipendekeza
orodha ya mambo ya Muungano ipungue na akayataja mambo ambayo yanapaswa
kubaki katika ushirikiano wa Muungano kuwa ni Ulinzi na Usalama, Uraia,
Sarafu, Mambo ya Nje, Usalama wa Anga, Benki Kuu, mambo ya hali ya
hatari, utabiri wa hali ya hewa na mengineyo.
Pia
alipendekeza uhusiano wa kimataifa kila nchi iwe na mamlaka yake ya
kusimamia eneo hilo sio kama ilivyo sasa ambapo mfumo uliopo sasa
umekuwa na malalamiko ya muda mrefu.
Nae
Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni(CCM), Salmin Awadhi Salmin
alitaka muundo wa sasa wa Muungano uendelee,lakini lazima Zanzibar iwe
na mamlaka yake,suala la uhusiano wa kimataifa lisiwe la Muungano,
Zanzibar iweze kuingia mikataba ya kimataifa, kujiunga na mashirika ya
kimataifa kama OIC na mengineyo.
“Muundo
wa sasa wa Muungano uendelee,lakini katiba ieleze wazi mamlaka ya
Zanzibar, Zanzibar iwe na mamlaka kamili katika Jamhuri ya Muungano
…katiba hii ya sasa haizungumzi mgawanyo wa madaraka, pia katiba ieleze
wazi zamu za Urais” Alisema Salmin.
Mwakilishi huyo aliongeza kwamba
إرسال تعليق