MNYIKA AHUTUBIA WAKAZI WA GOBA AWAELEZA UKWELI KUHUSU KERO YA MAJI

Leo ilikuwa siku nzuri sana kwa wapenzi na mashabiki wa Goba na vitongoji vyake walipo muona Mbunge wao J.J.Mnyika
akifunguka kwa kuwaeleza ukweli wananchi dhidi ya uongo wa magamba hasa hasa waziri wa maji aliposema maji yatatoka tarehe 20/2/13 lakini mpaka leo hakuna maji Goba.

Mnyika ametangaza rasmi kuwa tarehe 16/3/13 kutafanyika maandamano makubwa jijini Dar es salaam,kuelekea wizara ya maji kudai maji .

lakini mkutano wa leo umehudhuriwa na makamanda mbalimbali akiwemo Kileo,mzee Mkwesule,Diwani wa Ubungo ambaye ni kiongozi wa madiwani DSM,Ambaye alifunguka na kuwataja Diwani wa goba Kisoki,meya wa kinondoni,Diwani wa viti maalum Thereza ndiyo wanaohujumu upatikanaji na maji Goba

Ben Saanani hakuwa nyuma akatoa ukweli wa siri ya masalia

baadaye Mnyika akaeleza juu ya elimu yake kuwa hata kama mtu ana elimu kubwa au ndogo kinachozingatiwa ni uwajibikaji,uadilifu ,hekima na busara,ndiyo vinavyotakiwa .

Baadaye akatoa namba ya simu ya Prof Magembe 0786-034888 na ya naibu wake 0713-335733 watu wawapigie simu wawaulize waliahidi maji mbona kimya?






Post a Comment

أحدث أقدم