Halima Mdee akijibu moja ya swali aliloulizwa na Fina Mango
Mheshimiwa Halima Mdee akinukuu ilani ya
uchaguzi ya CCM wakati akijibu swali
Fina Mango akimuuliza Halima Mdee swali wakati wa mahojiano ya moja
kwa moja katika kipindi cha Makutano
Mtangazaji wa kipindi cha Makutano Fina Mango na Mbunge wa Kawe
Halima Mdee baada ya kipindi
----
Mbunge wa Kawe Mheshimiwa Halima
Mdee amesema watoto wa viongozi
kusoma shule za binafsi maarufu kama “Academia”
inachangia matokeo mabovu ya kidato cha nne kwa shule za
kawaida. Mdee
aliyasema hayo wakati akijibu swali la chanzo cha kushuka kwa kiwango
cha ufaulu
mwaka hadi mwaka wakati akiongea na Fina Mango katika Kipindi cha
Makutano. “Kwa
Mtazamo wangu mimi, zamani watoto wa viongozi tulikuwa tunasoma shule
hizi za
umma, kwa siku hizi tunawasomesha hizi shule za academia, kwa ubinafsi
wetu
hawa huku kwa kuwa watoto wetu hawapo hata ule moyo wa kutoa maelekezo
unakuwa
haupo” .
Mdee aliongezea kusema hii yote inachangiwa na mipango ya serikali iliyowekwa kwa kiwango kikubwa sana cha fedha kushindwa kutekelezeka au kusimamiwa ipasavyo ili yaweze kutekelezeka na kutolea mfano wa Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari.
(MMES II) ambao serikali ilitenga Shilingi bilioni 200 wakati huo kiwango cha ufaulu daraja la kwanza hadi la tatu ukiwa 37% ikiwa na malengo kiwango kipande hadi 70% lakini ilipofika 2009 kiwango cha ufaulu kikashuka hadi 17%, 2011 kikashuka tena hadi 9% na mwaka jana kikazidi kudidimia mpaka 5%. Mdee alisisitiza kuwa tatizo kubwa linalozikabili shule za kata ni miundombinu ya shule na maslahi ya walimu kwa kusema “Kinachojitekeza sasa ni mrundikano wa frustration za walimu, wamekata tamaa kabisa kwa sababu vipato vyao ni vidogo sana, lakini pamoja na kuwa vidogo vile wanavyotakiwa kuvipata kutokana na vipato kuwa vidogo hawavipati , na zaidi wakati walimu wanasema wanadai serikali inasema hawadai”.

Mheshimiwa Halima Mdee alimalizia
kwa kusema anadhani ni wakati
sasa kama taifa lazima serikali iamue inataka kufikisha wapi elimu kwa
kuwepo
bajeti inayotosheleza mahitaji na kuzingatia hali halisi ya maisha na
soko, na kusisitiza uwepo wa mitaala
inayoeleweka
tofauti na hivi sasa ambapo waalimu wanasema wanapokea maelezo tu na
kujiandalia wenyewe mitaala. Pia alisisitiza uwepo wa mgawanyo wa
walimu bila
upendeleo kwa kila shule tofauti na sasa ambako kuna shule hazina
walimu wa
kutosha na pia uwepo mamlaka ya usimamizi wa elimu yenye nguvu.
Mahojiano yote yanapatikana katika:www.hulkshare.com/ 81arza49bg5c
إرسال تعليق