Pamoja na kukidhi vigezo, 11% ya Wanafunzi wakosa mkopo Serikalini


Jumla ya wanafunzi 3,821 waliokuwa na sifa ya kupata mikopo katika elimu ya juu, hawakupata mikopo hiyo na hivyo kushindwa kuendelea na masomo yao, Bunge lilielezwa jana.

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philip Mulugo aitoa kauli hiyo jana alipokuwa akijibu maswali bungeni.

Alisema wanafunzi waliokosa mikopo ni asilimia 11.1 ya wanafunzi wote walioomba mikopo ambao walikuwa 37,315 kwa mwaka 2012/13.

“Hata hivyo, baada ya uchambuzi kwa wanafunzi 37,315 walioomba mikopo hiyo, wanafunzi waliobainika kuwa na sifa ya kupewa mikopo ni 34,140 lakini waliopata mikopo hiyo ni wanafunzi 30,319 sawa na asilimia 88.9 ya wanafunzi wote waliostahili kupewa mikopo hiyo,” alisema Mulugo.

Alikuwa akijibu swali la Rashid Ali Abdallah (Tumbe-Cuf) aliyetaka kujua ni kwa nini Serikali imeshindwa kuwapatia mikopo baadhi ya wanafunzi wenye sifa za kuendelea na masomo ya elimu ya juu.

Abdallah pia alihoji Serikali ina mpango gani wa makusudi wa kuhakikisha kuwa wanafunzi waliokosa mikopo hiyo wanapata elimu.

Naibu Waziri alisema, Serikali imetenga kiasi cha Sh 326 bilioni kwa mwaka 2012/13 kwa ajili ya kuwakopesha wanafunzi 95,902 wakiwamo wa mwaka wa kwanza ukilinganisha na Sh 56.1 zilizotengwa mwaka wa masomo 2005/06.

Gazebo la Mwananchi

Post a Comment

أحدث أقدم