Katibu
Mkuu wa wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Sethi Kamuhanda
akifungua mafunzo elekezi ya siku mbili kwa watumishi wapya wa wizara
hiyo leo katika ukumbi wa mikutano uliopo uwanja wa taifa jijini Dar es
Salaam.Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha wa 2012/13 imeajiri watumishi
wapya 30.
Mkurugenzi
wa Idara ya Utamaduni kutoka wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo Prof. Herman Mwasoko akiongea jambo wakati wa ufunguzi wa
mafunzo elekezi ya siku mbili kwa watumishi wapya wa wizara hiyo
yaliyofanyika leo katika ukumbi wa mikutano uliopo uwanja wa taifa
jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala Enely
Mwakyoma na kushoto ni Mkurugenzi wa Michezo Leonard Thadeo.
Mkurugenzi
wa Utawala na Rasilimali watu kutoka wizara ya Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo Barnabas Ndunguru akitoa maelezo kuhusu mafunzo
elekezi kwa watumishi wapya walioajiriwa na wizara hiyo kwa mwaka wa
fedha 2012/13 leo katika ukumbi wa mikutano uliopo uwanja wa taifa
jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa Sera na Mipango Gasper
Mwembezi.
Baadhi
wa waajiriwa wapya kutoka wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo wakimsikiliza katibu Mkuu wa wizara hiyo Sethi Kamuhanda (hayupo
pichani) wakati wa ufunguzi wa mafunzo elekezi yaliyofanyika leo
katika ukumbi wa mikutano uliopo uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.
Baadhi
ya wakurugenzi kutoka wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
wakimsikiliza katibu mkuu wa wizara hiyo Sethi Kamuhanda (hayupo
pichani) wakati akifungua mafunzo elekezi ya siku mbili kwa watumishi
wapya wa wizara hiyo leo katika ukumbi wa mikutano uliopo uwanja wa
taifa jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya
Habari (Maelezo) Assah Mwambene.
Katibu
Mkuu wa wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Sethi Kamuhanda
akiongea jambo leo na watumishi wapya wa wizara hiyo wakati wa mafunzo
elekezi yanayofanyika katika ukumbi wa mikutano uliopo uwanja wa taifa
jijini Dar es Salaam.Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha wa 2012/13
imeajiri watumishi wapya 30 ambao wengi wao ni vijana.
Mkurugenzi
wa Utawala na Rasilimali watu kutoka wizara ya Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo Barnabas Ndunguru (kulia) akimwambia jambo Katibu
Mkuu wa wizara hiyo Sethi Kamuhanda mara baada ya kumalizika kwa
ufunguzi wa mafunzo elekezi kwa watumishi wapya leo katika ukumbi wa
mikutano uliopo uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.
Waajiriwa
wapya kutoka wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo,
wakurugenzi wa Idara na Baadhi ya wafanyakazi wa wizara hiyo wakiwa
katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa ufunguzi wa mafunzo
elekezi leo uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam . Watatu kushoto
mstari wa mbele ni katibu Mkuu wa wizara hiyo Sethi Kamuhanda. (Picha na
Anna Nkinda – Maelezo).
Na Anna Nkinda.
Watumishi
wa Umma wametakiwa kufanya kazi zao kwa uadilifu, bidii na kujituma
huku wakifuata maadili ya kazi zao kwa kufanya hivyo wataweza
kutekeleza malengo ya Serikali ya kuwahudumia wananchi kama
wanavyotarajia kupata huduma nzuri.
Wito
huo umetolewa leo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo Sethi Kamuhanda, wakati akifungua mafunzo elekezi
ya siku mbili kwa wafanyakazi wapya yanayofanyika katika ukumbi wa
mikutano uliopo uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Kamuhanda
amesema kuwa uvumilivu unatakiwa mahali popote pa kazi na lazima
watumishi hao wawe na uwezo wa kukabiliana na changamoto watakazokutana
nazo kwa kufanya kazi kwa bidii na kujituma na siyo kukata tama, kwani
mtu akifanya kazi kwa bidii viongozi wake wataiona kazi anayoifanya na
kumuhitaji mara kwa mara.
Aidha
Kamuhanda amesema kuwa mtumishi wa sekta ya umma anafanya kazi ya
kuwatumikia wananchi bila ya kubagua wala kupendelea hivyo basi hapaswi
kuchagua kituo cha kufanyia kazi kwa kuwa hata wananchi walioko nje ya
miji wanatakiwa kupata huduma sawa na wananchi wa mijini.
Kamuhanda
amesema msiwe na tabia ya kuchagua maeneo ya kufanyia kazi kwani
mtumishi wa umma anapangiwa kazi na mwajiri wake katika kituo chochote
kile na huko mikoani ambako watumishi wengi hawapendi kwenda ndiko
ambako utajifunza mambo mengi zaidi na kuweza kukabiliana na changamoto
za kazi.
Katibu
Mkuu huyo pia amewasihi wafanyakazi hao kuwa na tabia ya kujifunza
kutoka kwa watumishi waliowakuta kazini wenye uzoefu wa kazi na
kutojifanya wajuaji kwani kwa kufanya hivyo watajiongezea ujuzi wa
kazi na kufika mbali zaidi.
Akitoa
maelekezo kuhusiana na mafunzo hayo, Mkurugenzi wa Utawala na
Rasilimali watu Barnabas Ndunguru amesema kuwa waajiriwa wapya
wanatakiwa kujua sheria, kanuni na taratibu zinazoendesha utumishi wa
umma.
Ndunguru
amesema, “Mafunzo elekezi kwa watumishi wapya Serikalini yanawawezesha
kupata ufahamu wa mambo mbalimbali kupitia mada zitakazofundishwa
ambazo baadhi yake ni majukumu ya wizara, maadili katika mtumishi wa
umma, wajibu wa kupiga vita rushwa mahali pa kazi na huduma kwa mteja”.
Alimalizia
kwa kusema kuwa mafunzo elekezi yatawawezesha watumishi hao kujitambua
kuwa wao ni watumishi wa umma na kwamba wanatakiwa kuzingatia maadili
ya utumishi wa umma na yataimarisha mahusiano kiutendaji kati ya
watumishi wapya, wakuu wa Idara na vitengo vyote na watumishi wote wa
wizara.
Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha wa 2012/13 imeweza kuajiri watumishi wapya 30 ambao wengi wao ni vijana kutoka kada mbalimbali.
Chanzo:- http://dewjiblog.com
إرسال تعليق