Rais wa zamani wa Pakistan Jenerali Musharraf akamatwa akijiandaa kugombea ubunge.

Polisi nchini Pakistan wamemtia mbaroni rais wa zamani wa nchi hiyo Jenerali Mstaafu Pervez Musharraf.
Musharraf amekamatwa leo nyumbani kwake mjini Islamabad na kufikishwa mahakamani.
Kiongozi huyo alirejea Pakistan mwezi uliopita, akitarajia kuwania ubunge katika uchaguzi mkuu mwezi ujao, baada ya kuwa uhamishoni kwa miaka minne.
Hata hivyo ombi lake lilikataliwa na maafisa wa uchaguzi, kwa misingi  kwamba anakabiliwa na mashitaka ya uhaini yanayohusiana na  kipindi chake cha utawala.
Hapo Jana mahakama mjini Islamabad iliamuru Musharraf akamatwe.

Post a Comment

أحدث أقدم