UJUMBE WA SAFARI LAGER WATEMBELEA BUNGENI MJINI DODOMA LEO

 Ujumbe wa Kampuni ya Bia Tanzania unaoongozwa na Meneja wa Bia ya Safari Lager,Oscar Shelukindo (pili kulia) ukiingia kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Mapema leo asubuhi kwa kuhudhuria Mkutano wa 11 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Wengine pichani toka kulia ni Mratibu wa Ziara ya Kombe la Ushindi wa Bia Bora Barani Afrika ulioupata Bia ya Safari Lager,Innocent Melleck,Mkurugenzi wa Miradi Maalum wa Kampuni ya Bia Tanzania,Phocas Laswai,Mpishi Mkuu wa Bia za TBL,Gaudence Mkolwe,Mkuu wa Mauzo wa Kanda ya Mashariki,James Bokela pamoja na Meneja Mauzo wa TBL,Kanda ya Kati,Julius Ngaga.Ujumbe huu upo mjini Dodoma kwa azili ya kupata Baraka za wabunge na uzinduzi rasmi wa Ziara ya Kombe la Ushindi wa Bia Bora Barani Afrika ulioupata Bia ya Safari Lager,ambapo jioni ya leo kutakuwa na tafrija fupi ya kupongeza ushindi huo itakayofanyika kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma.
Wakijadiliana jambo kabla ya kuingia kwenye ukumbi wa Bunge ili kufatilia shunghuli mbali mbali zinazoendeshwa na Bunge.
Wakiwa ndani ya ukumbi wa Bunge kufatilia shunghuli mbali mbali zinazoendeshwa na Bunge.

Post a Comment

أحدث أقدم