Dk.
Mwele Malekela ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa NIMR akifungua Mjadala juu
ya Utafiti wa udhibiti wa ugonjwa wa mabusha na matende kwa nchi za
Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika.
|
Na Mroki Mroki wa Father Kidevu Blog Arusha
Wilaya
94 zimefikiwa katika zoezi la unyweshaji dawa za Matende na Mabusha na
utoaji elimu linaloendeshwa chini ya Mpango wa Taifa wa Kudhibiti
magonjwa yasiyopea kipaumbele (NTD) unaoratibiwa na Wizara ya Afya na
Ustawi wa Jamii.
Mkurugenzi
Mkuu wa NIMR Dakta Mwelecele Malecela ameyasema hayo mjini Arusha
wakati akizungumza na waandishi wa Habari katika Kongamano la 27 la
taasisi hiyo la Sayansi la Kongamano la Pili la Afya Moja Afrika
linaloendelea mjini humo.
Dk.
Malecela amesema watu milioni 14 wamenufaika na huduma ya matibabu ya
mabusha na matende katika wilaya hizo 94 ambazo zimefikiwa katika zoezi
la ugawaji dawa na tiba.
Aidha
alieleza kuwa katika wilaya ya pangani jumla ya watu mia mbili
waliokuwa wanasumbuliwa na mabusha wamepatiwa tiba kwa njia ya upasuaji
na tayari wamerejea katika hali ya kawaida na kuweza kuendelea na
shughuli za maendeleo ya jamii yao.
Dk.
Malecela amesema Programu ya kudhibiti Metende na Mabusha imeandaa
mkakati maalum wa elimu kwa umma utakaowawezesha watanzania kupata elimu
na mbinu za kuwawezesha kushiriki harakati za kitaifa za kutokomeza
magonjwa hayo nchini ambayo yameleta hofu na mashaka katika jamii
kufuatia imani potofu.
Mkurugenzi
Mkuu huyo wa NIMR ameitaka jamii kushiriki katika zoezi la unyweshaji
dawa kwa miaka mitano mfululizo bila kuchoka ili kuweza kumaliza dozi na
hiyvo kuweza kujikinga na maambukizi na hatimaye kutokomeza magonjwa
hayo.
Dk.
Malecela amesema Wilaya ya Tandahimba, mkoani Lindi imefanikiwa
kupunguza wagonjwa wa matende na mabusha na kufikia kiwango cha chini
ya asilimia moja kutokana na jitihada za pamoja zinazoendelea za
kutokomeza magonjwa hayo chini ya Mpango wa Taifa wa Kutokomeza magonjwa
yasiyopewa Kipaumbele.
Pamoja mbu wa malaria aina ya Anopheles, ugonjwa wa Matende na mabusha pia huambukizwa kwa na mbu aina ya Culex.
Magonjwa
haya pia husababishwa na minyoo inayoishi kwenye damu na maji damu
ambayo husababisha madhara makubwa kwenye miguu ,matiti, mikono na
makende.
Mbu
aina ya Anopholes huweka mazalia yake katika maji yaliyotuama ambapo
Culex huweka mazalia yake katika maji machafu yakiwwemo yale katika
mashimo ya choo na madimbwi.
Aidha
Dk.Mwele amesema kuwa serikali imefanya jitihada kubwa sana kwani mfuko
wa rais wa kupambana na matende na mabusha umeonyesha mafanikio makubwa
na kuwezesha watu kupata matibabu kwa njia ya upasuaji.
Wagonjwa
480 wanatarajiwa kufanyiwa upasuaji wa mabusha katika mkoa wa Lindi
katika mwa huu, ambapo wagonjwa 54 kati yao wamekwishafanyiwa upasuaji
huo Mwezi April mwaka huu.
Baadhi ya washiriki ambao ni watafiti wakifuatilia mada za mjadala huo.
Dk.
Upendo Mwingira akitoa mada yake juu ya matumaini ya kutokomeza Ugonjwa
wa Matende na Mabusha hasa kufuatia utafiti wake Wilayani Tandahimba.
Mmoja wa watafiti
Sehemu ya washiriki wakifuatilia majidiliano hayo juu ya ugonjwa wa matende na Mabusha.
Watoa mada mbali mbali kutoka nchi za Afrika wakitoa mada zao juu ya Tathmini ya ugonjwa wa Mabusha na Matende katika nchi zao.
إرسال تعليق