Jambazi akiwa hoi katika hospitali ya Mwananyamala baada ya kupewa kichapo na wananchi wenye hasira kali.
KIJANA mmoja ambaye hajafahamika jina lake anayedaiwa kuwa ni jambazi
amenusurika kuuawa na wananchi wenye hasira kali eneo la Kimara jijini
Dar es Salaam. Kijana huyo akiwa na wenzake wawili waliokuwa na silaha
za moto tayari kwa kwenda kufanya uhalifu lakini kabla mpango wao
haujakamilika polisi waliingilia kati. Haikuwa kazi rahisi kuweza
kumkamata jambazi huyo kutokana na majibizano ya risasi kati yao na
polisi. Hata hivyo mmoja wao (pichani juu) alitiwa nguvuni wakati
wenzake wawili wakitokomea.
(Picha na Khatimu Naheka / GPL)
إرسال تعليق