Hussein
Machozi atakuwa chini ya usimamizi wa kampuni mpya ya nchini Kenya
iitwayo Candy n Candy ambayo pia imemsainisha Mr Nice. Akiongea, Machozi amesema mkataba huo umekuja wakati muafaka kwakuwa kwa
muda mrefu alikuwa anatamani kuwa chini ya menejimenti ya uhakika.
“Wenyewe watasimamia kazi zangu zote kiujumla kulingana kwa chochote kinachoingia kwa Machozi,” amesema.
“Jamaa watanifanyia kila kitu kuhusiana na studio, sehemu ya kukaa,
usafiri. Jamaa tumesaini kwa muda wa miaka mitatu. Siku nyingi sana
nilikuwa natafuta mtu wa kuwa karibu na mimi ilikuwa ngumu sana lakini
namshukuru Mungu jamaa wamepatikana na wako serious na mimi naamini
tutafanya kazi.”
Machozi amesema licha ya kuwa na uwezo mkubwa anashangaa jinsi baadhi
ya wadau wa muziki nchini wanavyomchukulia poa hadi watu wengine
tofauti wamesafiri kutoka Kenya kuja kumpa mkataba mzuri.
“Kila mtu ambaye nimekuwa nikimjaribu tufanye kazi watu wanakuwa
wazito. Mara nyingi huwa inaniwia vigumu kwamba labda watu hawanithamini
kwasababu siwezi ama? Kwakweli mawazo yangu kibongobongo yalikuwa
yameshaondoka. Ukiangalia kuna wasanii wengi ambao walikuwa na mawazo
yao kibongobongo na wamekishwa, tuko nao madereva wa bajaj sasa hivi
sasa sitaki hiyo hali inikute mimi. Inaniuma sana kuona watu wa nyumbani
kwangu wananichukulia poa halafu watu wa nchi jirani wananikubali,
inauma sana.”
Ameongeza kuwa anatarajia kuripoti Candy n Candy jijini Nairobi baada ya mwezi wa Ramadhan.
إرسال تعليق