Kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa:Balozi wa Vietnam Aagwa Rasmi Baada ya Kumaliza Muda wa Kazi Nchini Tanzania


 Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Angela Kairuki (katikati-mstari wa kwanza) akifuatana na Balozi wa Vietnam alimaliza muda wake wa kazi hapa nchini, Mhe. Nguyen Duy Thien (kulia), Mkuu wa Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini, Mhe. Balozi Juma Khalfan Mpango (kushoto mstari wa nyuma), Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora, Balozi Bertha Semu-Somi na Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Asia na Australasia, Bw. Omar Mjenga walipokuwa wanawasili katika Hoteli ya Hyatt Regency Kilimanjaro kwa ajili ya hafla fupi ya kumuaga Balozi Thien.
 Mhe. Kairuki akizungumza kuhusu uhusiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na Vietnam wakati wa hafla  hiyo huku Balozi Thien na Mkewe wakimsikiliza.

 Mkuu wa Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini Balozi Mpango nae akizungumza machache wakati wa hafla hiyo huku Mhe. Kairuki, Balozi Thien na wageni wengine waalikwa wakimsikiliza.
 Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Omar Mjenga akiwakaribisha wageni waalikwa kwenye hafla ya kumuaga Balozi Thien ambaye amemaliza muda wa kazi hapa nchini. Wengine katika picha ni Balozi Mpango na Balozi Semu-Somi.
 
Mhe. Kairuki akimkabidhi Balozi Thien na Mkewe zawadi ya picha ya kuchora ya Mji Mkongwe wa Zanzibar kama kumbukumbu yao kwa Tanzania.
Mhe. Balozi Nguyen Duy Thien na Mkewe wakimsikiliza Bw. Mjenga (hayupo pichani).
Picha na Reginald Philip.

Post a Comment

Previous Post Next Post