Uoza wa Utendaji Ndani ya SMZ
Jana
kulikuwa na mjadala mkubwa kuhusu bajeti ya Wizara ya Mawasiliano na
Miundo Mbinu, hususan katika utendaji mbovu wa wizara hiyo, ubadhirifu
wa mali ya umma, rushwa na wizi wa jumla wa mali ya umma. Wawakilishi
waliiweka ‘inbox’ wizara hii na hasa ujenzi wa Uwanja ‘mpya’ wa ndege wa
Zanzibar. Pesa nyingi zimeliwa, na kazi yote ni iliyofanyika ni mbovu
sana, sasa badala ya kujenga uwanja, SMZ inziba viraka vya run-way.
Yalipoibuka haya kwa wizara hii, na wizara nyengine zote takriban
zimetajwa kwa njia moja au nyengine na hali kama hii; ila mambo
kuzidiana.
Kilichonishangaza sana, ni kumuona Makamo wa Pili wa Rais, ambaye ni
mtendaji mkuu wa serikali katika baraza la wawakilishi, Balozi Seif Ali
Iddi akiwakingia kifua watendaji wabovu na wizara kama hii, inayonuka
uoza.
Alichokisema Makamo wa Pili wa Rais ni kuwa ‘SMZ itayafuatilia na
kuyafanyia kazi mapendekezo yote, malalamiko yote ya wajumbe wa BLW…..’
Hii ni kauli ya kila siku inakuwa hivi na huku watu wanaficha siri na
kuzidisha uoza, “wanafagia na kuweka taka chini ya Zulia”…….!
* Je, kuna scandal kama iliyoiukumba shirika la Umeme, na ushahidi upo wazi wazi (je, serikali imechukua hatua gani)
* Je, kuna uoza kuliko unaofanywa na ofisi ya mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali (CAG) kuanzia udokozi/wizi, hali nepotism(upendeleo) katika ajira, lazima uwe jamaa wa Fulani na Fulani ndio uajiriwe hapo, hata kama huna sifa za kitaaluma, lakini ‘sifa kuu ni unatoka wapi, na umezaliwa wapi, na wazee wako nani). Nafasi za masomo hapo kadhalika zinatolewa kwa misingi hiyo – mtu na mumewe, na mkwe, na mjomba wote wanafnya kazi ofisi moja, desk moja!
* Je, kuna scandal kuliko ya baraza la mji Zanzibar – ushahidi kamili, na Waziri Mwinyihaji Makame Mwadini, amekiri lakini kuondoka hataki, na serikali ya Shein haiwezi kumuondosha, na anajulikana kuwa ni ‘worn out’ na hafai.
* Kuna scandal kama ya wizara ya elimu, inajulikana na kila mtu kuhusu mishahara hewa na wafanyakazi hewa (ghost workers).Imekuwa NINI???
* Kuna zaidi kuliko rushwa inayotembea mahkamani au haki ya kupat cheti cha kuzaliwa/kufa – hiyo ni wizara ya abubakar khamis bakari (CUF) – huwezi kupata haki Zanzibar kama hujatoa rushwa — na majaji — watoto wetu, ndugu zetu na jamaa zetu wanayafanya haya ‘mchana’ bila kuogopa — iwe Ramadhan au mwezi wa kula mchana au makka au madina – ngoma draw. Wao ni pesa mbele kwa mbele.
* Kuna scandal kubwa sana wizara ya afya — wizara ya Juma Duni (CUF), wameleta dawa fake za kisukari, kinyume cha makubaliano na wafadhili wao ‘Danish government’. Kuna dawa za wagonjwa wa kili, ambayo chini ya makamo wa rais wa kwanza – bei yake ni kama 8-14 million, lakini hesabu inasema milioni 80/ — mpaka leo akina Juma Duni na Fatma Fereji wapo juu ya kiti cha raha na uwaziri.
* Ukiachilia scandals hizi na nyengine — utendaji mbovu nao umejaa, mawaziri wengi na watendaji wao hawaendi kazini – si huyo Nyanga tu kwa sababu ni mgonjwa bali hata hao waliokuwa wazima na afya zao imara. UTORO umekuwa tatizo kwa Zanzibar. Je, hali kama hii kweli itaifanya Zanzibar kusogea mbele kimaendeleo. Uongozi mbovu wa Shein na wasaidizi wake unazidi kuifisidi Zanzibar.

Nchi yeyote au jamii yeyote haiwezi kwenda mbele kama public
discipline haipo, Zanzibar imekumbwa na tatizo hilo – public discipline
ime – collapse, matokeo yake SMZ haina njia nyengine za kupata mapato
ila kuwakamua wafanya biashara hata anayeuza pipi, matokeo yake makubwa
zaidi, ni ukali wa maisha na gharama za maisha kwa watumiaji ambao ndio
sisi wananchi wa kawaida tunaoishi Kengeja, Tundauwa, Kitope, Kiboje,
Kangani Gae la Mtungi,Vitongoji, Darajani, Mkokotoni n.k ni mifano tu
hiyo –kama hakuna uazlishaji, utatumia nini??
Dr.Shein ‘wapige sindano watendaji wako’ tunataka tuone tiba halisi mara tu baada ya Eid, badilisha cabinet, inject new blood, na tuone matokeo yake – kuendelea kuwangangania akina Mwinyihaji, Duni, Shamhuna, Gavu, Haji Omar Kheri, Rashid Seif, Fereji, Nyanga, n.k hatufiki pahala.

إرسال تعليق