TANGAZO
Ubalozi
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania London unawakaribisha Watanzania
wote watakaoweza kupata fursa kuja kuzungumza na Waziri Mkuu, Mheshimiwa
Mizengo Kayanza Peter Pinda hapo Ubalozini siku ya Jumanne (tarehe 6
Agosti 2013) kuanzia saa Kumi na Nusu alasiri (1630 hours au 04.30
p.m.).
Katika
Mkutano huo, Mheshimiwa Pinda anatarajiwa kuzungumzia masuala
mbalimbali ya maendeleo ya nchi na ushirikishwaji wa Diaspora. Aidha
atajibu maswali kutoka kwa wananchi hao.
IMETOLEWA NA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI UINGEREZA, LONDON, JUMAPILI (4 AGOSTI 2013)
إرسال تعليق