Mheshimiwa
raisi, awali ya yote hongera kwa hotuba yako ya mwisho wa mwezi maana
ilijaa lugha tamu ya kidiplomasia inayo onyesha ni namna gani ulivyo
muungwana na usiye penda magovi au migogoro na nchi
majirani zetu kwenye ukanda wetu. Hotuba yako imeonyesha ni namna gani una dhamira ya dhati ya kuona utulivu una shamiri kwenye nchi majirani zetu.
Hotuba yako ilionyesha ukomavu mkubwa sana wa dhamira ya kuona amani ambayo ni tunda la haki ikitamalaki kwenye nchi za wenzetu, katika kipindi chako dhamira yako ulisha ionyesha na ukaitenda kwa vitendo nchi jirani ya kenya, ulifanya hivyo kwa Commoro na Madagascar, huko kote uliko toa ushauri wako hukuwahi kutukanwa wala kubezwa bali ulipewa sifa na kuonekana shujaa na hata ulipo amua kutumia vikosi vya majeshi yetu hakuna aliye hoji dhamira yako ya kuitafuta amani.
Kwa majirani zetu wa Rwanda imekuwa tofauti, wao ushauri wako kwao imekuwa nongwa, wamekubeza, wamekutukana, wamekunanga na wamefikia hata hatua ya kukutishia kukupiga.
Binafsi ulipo toa kauli kule Kagera kuwa majeshi yetu yako imara na mipaka yetu iko salama huku ukitahadharisha atakaye leta chokochoko kukiona cha mtema kuni nilijua unajibu mapigo kwa Kagame, kumbe hukuwa na maana hiyo wala dhamira hiyo, niliogopa nikajua unataka twende tukamchape Kagame. Mungu ashukuriwe hekima ya kidiplomasia bado iko kifuani pako japo mwenye jicho la tatu akikusoma katikati ya mistari anaona fukuto lisilo kuwa na afya kati yako na kagame.
Hata hivyo, baada ya kusikiliza hotuba yako, leo nataka kuwa mshauri wako kuhusiana na dharau, matusi na dhihaka zilizo onyeshwa na wanyarwanda, kwako na kwetu sisi watanzania, najua una washauri wengi
na wabobezi kwenye mambo mbalimbali ya kiuchumi, kisiasa, kitamaduni, kijamii na hata kiimani, najua

washauri wako wanafanya kazi yao vizuri usiku na mchana kwa weledi na kwa ufanisi wa hali ya juu.
Busara imenituma kukushauri, mimi ni muungwana wa kijiwe cha kahawa nisiye kuwa na wadhifa wala hadhi ya kukuona ninapo jisikia kufanya hivyo kwa muda wowote lakini najua nina uwezo wa kukufikia kwa njia ya
maandishi ambayo kwangu ina nguvu kuliko kuja kubisha hodi kwenye nyumba tuliyo kupangisha.
Kabla sija kushauri naomba nianze kwa kunukuu maneno yako kwenye hotuba yako ya mwisho wa mwezi, umesema "Ushauri si shuruti, ushauri si amri, una hiyari ya kuukubali au kuukataa" kwa heshima na taadhima
naomba ushauri huu ninao kupa wewe usiukatae kwa sababu eti si shuruti au amri. Wewe nifanye mimi mjinga na upokee tu maana nataka kukuepusha na kikombe cha matusi na dharau kutoka kwa viongozi wa nchi nyingine ambao huenda baadae ukajisikia kuwashauri kama ilivyo tokea kwa Kagame na wao kuamua kufuata mkondo aliofuata Kagame na kuamua kuporomosha matusi na kejeli kwetu halafu dunia nzima ikajua tena kuwa ile nchi ya Nyerere iliyokuwa inaheshimika sasa hivi imekuwa ubao wa matusi na kejeli. Wapo watakao sema Nyerere amekufa na heshima ya nchi yake na walio baki wote ni dhaifu tu! japo inawezekana kuna wadhaifu wachache.
Mheshimiwa raisi, kipindi hiki achana kabisa na nia au dhamira ya kutoa ushauri kwa kiongozi yoyote mwenye nchi yenye mgogoro wa amani, natambua unajua kuwa amani ni tunda na zao la haki bali amani si tunda
na zao la maombi kama baadhi ya viongozi wa chama chako wanavyo potosha. Lakini pia natambua kuwa haki ina mbegu ya upendo ndani yake. Hivyo kabla hujatenda upendo kwa mtu mwingine lazima ujipende kwanza wewe mwenyewe na kabla ya kuonyesha njia ya haki ni lazima wewe mwenyewe ujitendee haki na kuonyesha kweli kuwa haki imetendeka.
Msingi wa mimi kukushauri usimshauri tena kiongozi mwingine wa nchi nyingine umelala kwenye mafundisho ya dini zetu tunazo ziabudu, dini zote zinatabia moja kuu, zinafundisha upendo na kutendeana haki huku
zote zikiamini kuwa haki ndio msingi wa upendo na amani.
Mafundisho ya dini yanatufundisha kuusema ukweli hata kama uta umiza vishikizo vya mioyo yetu, lakini pia mafundisho hayohayo yanatufundisha kuondoa kibanzi kwenye macho yetu kabla hatuja fikiria kuondoa boriti kwenye macho ya wenzetu, hii ni misingi muhimu sana tuliyo wekewa kwenye mafundisho ya dini zetu na naamini ni udhaifu wa kutokufuata mafundisho haya ndio kumesababisha wanyarwanda kutudharau,
kukudharau wewe na hata kukutukana kama nilivyo kusikia ukilalamika.
Katika kipindi cha uongozi wako hasa n'ngwe hii ya mwisho kumekuwa na matukio mabaya sana naya Kuogofya ambayo pia naamini hata shetani ametushangaa sisi kama watanzania kwa matukio mabaya yaliyotokea na kuwa tabia ambayo hatukuwa nayo mwanzoni! Wapo watanzania wenzetu walio uwawa au kupoteza maisha mikononi mwa polisi, kumetokea vifo vingi vyenye utata, kuna watu walitekwa, wameteswa na kung'olewa meno na kucha bila hata ganzi haya yote yametokea na sauti za Watanzania zikapazwa lakini jitihada zako za dhahiri za kukomesha vitendo hivi hazija onekana kwa dhati. Ndio maana nikasema nikushauri kwa dhati ya moyo wangu ili uhakikishe kwanza haki inatendeka nyumbani kwako kabla
ya kwenda kushauri kwenye nyumba ya Kagame.
Japo kabla yako nilisha hadithiwa kuwa yaliwahi kutokea mauwaji ya Mwembe chai na vurugu za uchaguzi wa zanzibar ambazo zilisababisha vifo vya makumi na wakimbizi kule shimoni (mombasa) nchini Kenya
wakati wa mzee mkapa lakini pamoja na hayo nimejikuta najiuliza maswali.
Raisi wangu, dawa pekee ya kuepuka matusi na kejeli na kutuepusha sisi na kikombe cha kejeli dhidi ya mataifa mengine achana na habari za kutoa ushauri kwa wengine, tukae chini tumalize matatizo yetu, tutoe
boriti kwenye jicho letu ndio turuke kiguu na njia kwenda kuwa shauri wengine wenye matatizo. Kaa chini utatue sintofahamu ya Mtwara na ikiwezekana anza hapo hapo ikulu kwa kuwauliza walio tangazia taifa
kuwa viongozi wa CUF walio pata kibao kutoka kwa wanajeshi kule Mtwara eti ni vibaka, ikulu yako ina halalisha vibaka wale mkong'oto na sio kufikishwa kwenye vyombo vya sheria?!
Mheshimiwa, Sisi yetu yanatushinda kwa nini tuwe na upendo wa mshumaa wa kumulikia wengine huku tukiteketea?! Amani yetu inapotea kutokana na haki kukandamizwa kwa nini tusijenge misingi na nguzo imara za haki zitakazo simika amani ndio tutoke kwenda kushauri wengine na wengine watakao taka waige kutoka kwetu?
Chukua ushauri wangu ninao utoa kutoka kwenye sakafu ya moyo wangu na kwa kuwa tuko kumi la mwisho la mwezi mtukufu wa ramadhani kabla ya kufungua kwa sikukuu ya eid nikutakie funga njema na Eid Mubarak
Sheikh Jakaya Mrisho Kikwete.
--- Mohamedi Mtoi

- Umethubutu vipi kwenda kumshauri Kagame apatane na waasi wakati wewe umeshindwa kutekeleza ombi la muda mrefu la barua ya chama hasimu (chadema) kwa chama chako kuhusu kuunda tume huru ya kimahakama itakayo ongozwa na majaji kuchunguza vifo vyenye utata vilivyo tokea kwenye mikutano ya chama hicho pamoja na vifo vingine vyenye utata?!
- Umethubutu vipi kwenda kumshauri kagame wakati wewe ni amiri jeshi mkuu wa majeshi na jeshi lako la polisi kwenye ripoti mbalimbali linaonekana kuwa ni jeshi ambalo linakiuka haki za raia ikiwemo kubambikiza kesi na kutunga mashtaka ya uongo na kesi za ugaidi ambazo hazipo? Ulisha kaa na Polisi kama amiri jeshi mkuu kukomesha tabia hii ili litende haki kwa watanzania?
- Umepata wapi uhalali wa kimaadili (moral authority) kutumia busara kumshauri Kagame aongee na wakinzani wake kisiasa wakati wewe umeshindwa japo kukaa na viongozi wa upinzani husasi chadema
- kujadilina nao na kujua sababu za wao kukamatwa mara kwa mara na kuwa na kesi za mfululizo zisizo kuwa na kichwa wala miguu huku jeshi la Polisi likiwaandama kuliko linavyo wandamana na kuwanyamazia viongozi wa ccm hata wanapo toa kauli zenye utata?!
- Nimejiuliza, umepata wapi mamlaka ya kimaadili kumshauri Kagame aongee na waasi wapinzani wakati wewe kupitia hotuba yako ya mwisho wa mwezi ulisha wahi lalamika kuwa chadema wanafanya maandamano ili kuondoa serikali iliyoko madarakani kihalali kama ilivyo tokea Misri na Libya huku ukiwa hujawahi kukaa na chadema hao hao ukawauliza kama ni kweli walikuwa na mpango huo?! Na mlifikia muafaka gani ili wauache mpango wao maana uliwatahadharisha wananchi juu ya maandamano ambayo ni haki ya kiraia?
- Bado najiuliza, umepata uhalali gani wa ki-maadili kumshauri Kagame aongee na wapinzani waasi wakati wewe umeshindwa japo kuwapa pole chadema (chama pinzani hapa nyumbani) ambao ni wahanga walio lipuliwa mabomu kwenye mikutano yao kadha huku wewe ukikaa kimya na kushindwa kutoa japo pole wakati si kawaida yako kwenye mambo ya misiba?!
- Naendelea kujiuliza, umepata uhalali gani wa kimaadili kumshauri Kagame aongee na wapinzani waasi wakati waziri wako mkuu akitoa amri zenye utata mara kadhaa kupitia bunge?! Mara anaye uwa albino naye auwawe, mara "liwalo na liwe", mara "wapigwe tu maana sasa tumechoka" hivi nyinyi mlio choka mnatoaje ushauri kwa wengine ambao hawaja choka?!

إرسال تعليق