Chama cha RPF nchini Rwanda kinaelekea kupata ushindi mnono katika uchaguzi wa bunge uliofanyika jana

Wananchi wa Rwanda kipiga kura
Na Ali Bilali

Chama cha RPF cha Rais wa Rwanda Paul Kagame kinaelekea kupata ushindi wa kishindo katika uchaguzi wa wabunge uliofanyika jana nchinihumo na ambao unaendelea leo kwa kuwachaguwa wawakilishi 24 wa kike. Uchaguzi huo umeanza jana jumatatu na unaelekea kutamatishwa kesho baada ya kuchaguliwa wa wawakilishi watatu wa walemavu.


Muungano wa vyama unaoongozwa na Chama cha RPF cha rais Paul Kagame unaelekea kupata ushindi katika uchaguzi huo ambapo kiasi ya kura ambazo zimekwisha hesabiwa chama hicho kimejipatia asilimia 76 ya kura baada ya matukio ya awali ya uchaguzi huo.

Kwa mujibu wa matokeo yaliwekwa bayana na tume ya kitaifa ya uchaguzi NEC, Chama cha RPF na washirika wake wamepata kura 3.395.962 kati ya 4.462.917 zilizo pigwa. Wananchi wasiofikia milioni sita walikuwa wamejiorodhesha katika daftari la wapiga kura ambapo mkuu wa NEC Kalisa Mbanda anasema kuwa matukio hayo ya awali ni sawa na asilimia 60 ya wapiga kura.

Chama cha PSD kimepata asilimia 13.01 huku chama cha PL kikipata asilimia 9.38 ya kura ambazo zimekwisha hesabiwa.

Chama cha PS-Imberakuri kinachukuwa nafasi ya tatukwa asilimia 0.56 ya kura kikkifuatiwa na wagombea binafsi wanne wote wakiwa na asilimia 0.5 ya kura.

Vyama vya RPF, PSD na PL ndivyo ambavyo vitakuwa na wawakilishi bungeni ambapo ndivyo vinazidi asilimia 5 ya kura inayoagizwa ili viwakilishwe bungeni
kutokana na tofauti iliopo na idadi ya kura ambazo zimekwisha hesabiwa, matokeo hayo huenda yasibadiliki sana.


kwa mujibu wa tume ya kitaifa ya uchaguzi NEC, huenda pasiwi na mabadiliko makubwa ya matokeo hayo, kura za raia wa Rwanda wanaoeshi nje ya nchi ndizo pekee ambazo zinaweza kubadili matokeo.

Wachambuzi wa maswala ya siasa wanasema kuwa Vyama vya PSD na PL ambavyo vinashiriki katika serikali ya rais Kagame ni vibaraka wa chama tawala ambavyo vipi kwa ajili ya kubaini kuwa kuna mfumo wa vyama vingi nchini Rwanda.

Chama cha PS-Imperakuri cha rais wa zamani Bernard Ntaganda alieko korokoroni tangu mwaka 2010 kwa tuhumu za kutaka kuyumbishas usalama wa taifa na ubaguzi, nacho pia kinashukiwa kimepata ulaghai kutoka chama tawala cha RPF.

Matokeo ya sasa hayapishana sana na yale ya mwaka 2008 ambapo chama cha RPF kilipata asilimia 78.7 ya kura dhidi ya asilimia 13.12 ya chama cha PSD na asilimia 7.5 ya chama cha PL.

Post a Comment

أحدث أقدم