Mawaziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry na wa Urusi Sergei Lavrov
Reuters
|
Marekani na washirika wake waendelea kusisitza juu ya uwepo
wa azimio kwenye baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu matumizi
ya bomu za sumu nchini Syria na kuitishia serikali ya rais Assad kuhusu
madhara yatayoweza kujitokeza kama itashindwa kuheshimu majukumu
yake. Serikali za Washington na Paris zinazingatia ripoti ya wataalam
wa Umoja wa Mataifa kuhusu matumizi ya bomu za kemikali iliotolewa jana
Jumatatu kwamba kuna ushahidi mkubwa wa matumizi ya bomu aina ya
sarin Agosti, 21, na kuiweka hatiani serikali ya huko Damascus.
Waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei
Lavrov ambaye serikali yake inapinga vikali uwepo wa azimio lolote
kwenye baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu Syria, anakutana kwa
mazungumzo na mwenziwe wa Ufaransa Laurent Fabious.
Wakati huo huo rais wa Ufansa Francois Hollande
anakutana na waziri wa mambo ya nje wa Qatar Khaled Attiyah ambapo
watajadili kuhusu mzozo wa Syria
Ikulu ya Marekani imesema jana Jumatatu kuwa
ripoti ya Umoja wa Mataifa juu ya matumizi ya bomu zenye kemikali nchini
Syria mwezi uliopita inaonyesha kuwa serikali ya Bashar al-Assad
inahusika.
Msemaji wa Ikulu ya White House Jay Carney amesema
ripoti hii, inaonyesha kwamba silaha zenye kemikali zilitumiwa na
ambazo huwezi kuzitumia bila kuwa na vifaa maalum na ambavyo serikali
pekee ndiyo inavyo vimiliki
Wataalam wa Umoja wa Mataifa ambao walipewa jukumu la kuendesha
uchunguzi kuhusu matumuzi ya silaha zenye kamikali katika shambulio la
Agosti 21 nchini Syria ambayo yaligharimu maisha ya watu zaidi ya 1400,
ripoti ambayo ilitolewa jana inaonyesha ushahidi wa kutosha wa uwepo wa
matumizi hayo.
Katika Ukurasa wa kwanza wa ripoti, hiyo
ilikanbidhiwa kwa Katibu Mkuu Ban Ki-moon na mkaguzi mkuu Sellström Aake
inaonyesha kuwa silaha za kemikali zilitumika kwa kiwango kikubwa
katika mgogoro unaendelea nchini Syria na ambapo waathirika ni raia,
lakini pia watot
إرسال تعليق