Mpishi mnene kupindukia apata afueni

New Zealand ina idadi kubwa sana ya watu walio wanene kupita kiasi
Mwanamume mmoja raia wa Afrika Kusini aliyekuwa anakabiliwa na tisho la kufukuzwa kutoka New Zealand kwa kuwa mnene kupita kiasi,ameongezwa muda wa miezi 23 kuendelea kuishi nchini humo.
Hata hivyo,Albert Buitenhuis hatapokea huduma ya bima ya afya ya serikali.
Albert ambaye ni mpishi wa hoteli, ana uzani wa kilo 130 na alikata rufaa miezi miwili iliyopita baada ya ombi lake la kutaka apewe viza mpya ya kumwezesha kufanya kazi nchi humo kukataliwa kwa misingi kuwa afya yake sio nzuri.
Amepunguza kilo 30 tangu kuhamia mjini Christchurch miaka sita iliyopita.
Naibu waziri wa uhamiaji Nikki Kaye alisema kuwa sababu kuu ya ombi la Bwana Buitenhuis kukataliwa ni ugonjwa alionao kwenye magoti yake.
Hata hivyo, aliwapa muda zaidi Bwana Buitenhuis na mkewe Marthie, wa kuweza kuishi nchini humo baada ya kusema kuwa itambidi agharamie matibabu yake mwenyewe.
Aidha Bwana Buitenhuis, aliyeandika kuhusu masaibu yake kwenye blogu, alisema kuwa hatua ya serikali imeleta hisia mchanganyiko kwake.
Buitenhuis, ameahidi kupunguza kilo nyingine 25 ingawa kwa sasa anasema kuwa wanakabiliwa na changamoto nyingi kwani hawana pa kuishi.
New Zealand ni moja ya nchi yenye idadi kubwa ya watu walio wanene kupita kiasi.
Idara ya uhamiaji imesema kuwa ni muhimu kuwa wahamiaji wote wawe na hali ya kiafya inayokubalika ili kuipunguzia serikali gharama ya kutibu wagonjwa.
- bbc

Post a Comment

أحدث أقدم