Mwanzilishi
wa style ya ‘Takeu’ Lucas Mkenda a.k.a Mr Nice ameingia tena kwenye
mgogoro na meneja wake mpya wa Candy & Candy baada ya
kutokukubaliana baadhi ya mambo aliyokuwa akishauriwa na lebo hiyo.
Akizungumza na MWANANCHI mkurugenzi wa Kampuni ya Candy & Candy
Records, Joe Kariuki alisema kampuni yake na Mr Nice anayependwa nchini
Kenya walitofautiana katika baadhi ya mambo hasa ubora wa kazi.
“Mr Nice ni msanii anayependwa sana hasa Mombasa, lakini wiki chache
zilizopita tulikuwa na mabishano kidogo hii ilitokana na mtazamo tofauti
hasa ni kutokana na wimbo wake mpya wa ‘Akina Mama’ binafsi ule wimbo
sikuupenda na nilimshauri kwamba ni vyema tungetumia wimbo mwingine,
lakini aling’ang’ania”
Aliendelea kusema “Wimbo ule tuliupiga katika vyombo vya habari kwa
bahati mbaya haukufanya vizuri lakini nilimtahadharisha mapema.
Kariuki aliongeza “Kampuni inaweza kupata hasara, lakini tumeamua
kuendelea na mkataba kwani kwa sasa ameelewa na tunakwenda kama kampuni
inavyotaka,” alisema Kariuki kampuni hiyo imeingia mkataba na wasanii
wengine kutoka nchini Tanzania wakiwamo Four – D, Top C, Mr Nice na Baby
Madaha
Mr Nice hapo awali alikuwa na mkataba na lebo ya GrandPa Records
ambayo walishindwana na kuamua kuvunja mkataba na sasa yupo na Candy
& Candy Records
إرسال تعليق