Rama Dee na Cpwaa wathibitisha kuwa Kuingiza hela kupitia mauzo ya iTunes inawezekana,

998895_677924815570358_1954277516_n 
Kama wewe ni mmoja wa watu wanaohisi kuwa ni ngumu kwa shabiki wa muziki wa Tanzania kulipa dola 0.99 ambazo ni sawa na shilingi 1,600 au dola 1.69 ambazo ni zaidi zaidi ya shilingi 2,700 kununua wimbo iTunes ni ngumu, basi huenda ukawa huujui ukweli.
Inawezekana sana kwa msanii wa Bongo kupiga mkwanja kupitia mauzo ya kidigitali na Rama Dee na Cpwaa ni mfano mzuri.Wote wameingiza albam zao na kuziuza iTunes na maendeleo yanaridhisha huku wakidai inawezekana kwa msanii wa Tanzania kupata hela huko.
“Inawezekana kabisa maana nje kuna Watanzania wengi sana na wanataka kazi za Watanzania,” Rama Dee ameiambia Bongo5 na kuongeza kuwa ripoti ya mauzo yake kwenye Itunes itatoka hivi karibuni kuonesha kiasi gani ameingiza tangu aanze kuuza nyimbo za albam yake yenye nyimbo 12, The Best of Rama Dee 2000-2013.a
“Tanzania kinachotusumbua wasanii ni jinsi ya kumfikishia shabiki kazi ila kiukweli pande zote zina mauzo mazuri kabisa,” ameongeza.
Kwa upande wake Cpwaa, jana kupitia Facebook aliandika:
Nimetoka kucheki sales report ya mauzo ya nyimbo zangu kwenye digital stores,nafarijika kuona kuna watu wamenunua kazi zangu hasa kupitia iTunes wengi kutoka UK na US. Naomba tuendelee kupeana support huo mtonyo ni pensheni ya uzeeni na utakuja kusomesha watoto baadae.”
Msanii anawezaje kuingiza nyimbo zake iTunes? Rama Dee anafafanua:
Lazima uwe na credit card na uwe na zip code. Unalipia kuweka album iTunes, US dollars na unapewa account ambayo unapewa habari zote kuwa watu wangapi wameingia, wamesikiliza na kununua.”
Unaweza kununua nyimbo kwenye albam za Rama Dee na Cpwaa kwa kubonyeza link hapo chini.

The Best of Rama Dee 2000-2013


Pwaa “the Album”

Post a Comment

أحدث أقدم