Ronaldo aongeza mkataba Real Madrid; Sasa ni mchezaji anayelipwa zaidi duniani

 
Picture
Cristiano Ronaldo (2nd L) puts on his glasses before posing alongside Real Madrid president Florentino Perez (L) and Real Madrid board of management member Fernando Fernandez Tapias (R) after signing a contract renewal for Real Madrid at Estadio Santiago Bernabeu on September 15, 2013 in Madrid, Spain. (September 14, 2013 - Source: Gonzalo Arroyo Moreno/Getty Images Europe)
Mshambuliaji wa klabu ya soka Real Madrid ya nchini Uhispania, Christian Ronaldo, Jumapili ya leo aliongeza mkataba mwingine wa kuitumikia klabu hiyo mpaka kufikia mwaka 2018 huku akiwa ni mchezaji anayelipwa ghali zaidi duniani.

Kuongeza mkataba kwa mshambuliaji huyu kunafuta uvumi uliokuwepo awali kuwa nguli huyo angeihama 
klabu hiyo na kujiunga na klabu za nchini Ufaransa ambazo zilionesha nia ya kumnasa mchezaji huyo.

Christian Ronaldo ameongeza mkataba wa miaka mitano kuitumikia klabu yake ya Real Madrid mkataba ambao unamaanisha kuwa mshambuliaji huyo huenda akamalizia soka lake klabu hapo.

Mchezaji huyu anatarajiwa kupokea mshahara wa kiasi cha Euro milioni 20 kwa msimu na kumfanya kuwa  mchezaji anayelipwa ghali zaidi duniani akifuatiwa na mpinzani wake anayekipiga klaby ya FC Barcelona, Lionel Messi anayelipwa Euro milioni 16 kwa msimu.

Ronaldo ambaye uhamisho wake ulivunja rekodi ya dunia wakati alipojiunga na timu hiyo akitokea Manchester United ya nchini Uingereza kwa dau la Euro milioni 90 mwaka 2009 ambapo amefanikiwa kufunga mabao 203 kwenye mechi 203 alizocheza.

Kwenye mkutano wake na waandishi wa habari wakati akitangaza kumuongezea mkataba mchezaji huyo, rais wa Real Madrid, Florentino Perez amesema kuwa wanajivunia kuwa na mchezaji mwenye kiwango kama Chrisian Ronaldo na wanafuraha kumbakiza mchezaji huyo. -- Emmanuel Richard Makundi, RFI

Post a Comment

أحدث أقدم