Serena Williams afikia rekodi ya Roger Federer


TEN-US OPEN-WILLIAMS-AZARENKA
Na.Mo Blog Team
Mcheza tenisi wa kike namba moja duniani, Serena Williams, amefikia rekodi ya Roger Federer ya kushinda mashindano mengi kwa wanaume baada ya kumshinda mchezaji namba mbili duniani, Victoria Azarenka, katika mchezo uliochukua muda mrefu kwa kipindi cha zaidi ya miaka 30 kwenye mashindano ya wazi ya US.
Williams allifikia rekodi hiyo kushinda vikombe vikubwa 17 kwa ushindi wa seti 7-5 6-7 (6-8) 6-1 katioka mchezo uliodumu kwa masaa mawili na dakika 45 uliochezwa Jumapili.
“Yeah, hii safi sana,” alisema Williams baada ya kuifikia rekodi ya Mswisi Federer.
Willimas mwenye umri wa miaka 3, pia amekuwa mwanamke mwenye umri mkubwa kushinda mashindano ya wazi jijini New York, ikiwa ni siku 293 zaidi ya umri wa Margaret Smith Court ambaye alishinda mwaka 1973.
Williams amepata dola za Kimarekani milioni 3.6 pamoja na nyongeza ya dola za Kimarekani milioni moja kwa kufanikisha matukio kabla ya mashindano hayo.

Post a Comment

أحدث أقدم