SMZ: Hakuna tatizo Azzan kutibiwa nje

Sheikh Azzan Khalid Hamdan
Na Mwiny Sadallah

Waziri wa Afya wa Zanzibar, Juma Duni Haji, amesema hakuna tatizo kwa kiongozi mwandamizi wa Uamsho, Sheikh Azzan Khalid Hamdan, kutibiwa nje ya nchi kama jopo la madaktari litapitisha uamuzi huo.
Akizungumza na Mwananchi Ofisini kwake Vuga mjini Zanzibar juzi, Duni alisema kwa mujibu wa katiba, mwananchi yeyote ana haki ya kutibiwa nje ya nchi kwa maradhi ambayo tiba yake haipatikani nchini.

Alisema hata hivyo hatua hiyo itategemea uwezo wa Serikali kifedha na ukubwa wa ugonjwa.
“Bado sijapokea ripoti kuhusu Sheikh Azzan, wajibu wangu ninapopokea nalazimika kupeleka Hazina, hakuna ombi hata moja nililowahi kulitupa,”alisema waziri.

Alisema daktari anayemtibu sheikh huyo, anapaswa kuwasilisha ripoti ya mgonjwa katika Bodi ya Matibabu ya Nje ambayo ndiyo yenye uamuzi wa mwisho kulingana na ukubwa wa ugonjwa.


Alisema ingawa Sheikh Azzan ni mshtakiwa, hicho hakiwezi kuwa kigezo cha kukosa kutibiwa nje.
Kiongozi huyo amelazwa katika Hospitali ya Mnazi Mmmoja mjini Zanzibar akisumbuliwa na maradhi ya figo kuwa na vijiwe na anapaswa kupelekwa nje ya nchi kwa matibabu.

Katibu wa hospitali hiyo, Omar Abdallah Ali alisema kwa utaratibu Bodi ya Matibabu ya Nje inakutana kila baada ya miezi miwili kufanya uamuzi kuhusu wagonjwa wanaotakiwa kutibiwa nje ya nchi.

Alipia pia inaweza kukutana kwa dharura pale panapokuwa na mgonjwa anayehitaji uharaka wa matibabu.
Kiongozi huyo wa uamsho anakabiliwa na mashtaka ya kufanya uchochezi na kusababisha uharibifu wa mali za mamilioni ya fedha.

Chanzo - Mwananchi

Post a Comment

أحدث أقدم