Wanaume wanaomiliki wanawake -mmoja anakuwa na zaidi ya 6.


ombiOmbi Sanga ambaye ni Mhudumu wa Afya ya msingi katika kijiji cha Ivalalila. Picha na Herieth Makweta.
Hii ni sehemu ya pili ya makala kuhusu Kijiji cha Ivalalila wilayani Makete, Mkoa wa Njombe ambapo pamoja na mambo mengine ilieleza namna wanaume wa eneo hilo wanavyomiliki wanawake zaidi ya watano bila kujali athari zake.
Wapo wanaume wanaosaidia lakini si wote. hapa kijijini kuna mambo mengi yasiyo mazuri hasa kuhusu suala la jinsia. Mwanamke anachukuliwa kama chombo cha starehe na mtumwa.”
Wanaume wanasemaje
Efedi Eskaka Chaula (40), anakiri kuwapo na tabia ya wanaume kumiliki wanawake zaidi ya sita akisema: “Ni kweli, wanaume tuna wanawake wengi hapa kijijini, lakini si kwamba wanaume ndiyo wanatafuta wanawake ingawa wapo wanaorithi wajane wa kaka zao au wadogo wao.
Ukweli ni kwamba wanawake wengi wanawahonga wanaume, ndiyo maana nao wanalazimika kuwa na wanawake wengi. Hata hivyo ni kama mila na desturi za kurithi na mitindo ya maisha kwa hapa kijijini.”
Naye kijana aliyeomba kutambulika kwa jina moja la Peter ( 21) anasema: “Mimi nina wanawake saba, wawili ni wasichana wadogo wanasoma sekondari na hawa watano ni wakubwa sana tu. Hawa wananipa fedha, zinanisaidia kumpa msichana ninayempenda, huyu mwingine natembea naye tu.”
makala haya kuhusu Kijiji cha Ivalalila wilayani Makete, Mkoa wa Njombe ambapo pamoja na mambo mengine ilieleza namna wanaume wa eneo hilo wanavyomiliki wanawake zaidi ya watano bila kujali athari zake. Leo tunawaletea sehemu ya mwisho.
Alipoulizwa kama anafahamu kuhusu gonjwa la Ukimwi Peter alijibu: “Kwa kweli najua, ila nimekata tamaa kwani najua lazima nimeathirika, sijawahi kupima kwa hiari ila kuna wanawake niliotembea nao zamani sana nikiwa na miaka 14 walishafariki kwa Ukimwi, hivyo na mimi najua ninao.”
Alipoulizwa iwapo ana ndoto za kuoa, Peter anajibu: “Nampenda sana msichana mmoja, lakini siwezi kuoa kwa kuwa najua atapata mimba na akienda kupimwa itagundulika kuwa ana Ukimwi hivyo ninaweza kufa haraka.”
Anasisitiza kuwa wanaume wengi waliopima na kugundulika na Virusi vya Ukimwi hufa haraka.
Hata hivyo Peter ni tofauti na Eliudi(26), anayedai kuwa wanawake wengi kijijini hapo wanaongea sana.
“Wanawake wengi wanaongea sana, wana gubu. Hili ndilo lililonihamisha kwa mke wangu wa awali na kuanza kuambatana na wanawake wengine,” anasema Eliud aliyekataa kutaja idadi ya wanawake alionao.
Chanzo:Mwananchi

Post a Comment

أحدث أقدم