Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo.
Na Sharon Sauwa,Mwananchi
Dodoma.Serikali bado haijaamua
utaratibu utakaotumika katika kupanga madaraja ya watahiniwa wa mitihani
ya kidato cha nne iliyofanyika mwaka huu.
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,
Philipo Mulugo alisema juzi jioni katika Viwanja vya Bunge kuwa, uamuzi
juu ya utaratibu utakaotumika kupanga matokeo hayo utaamuliwa katika
vikao vya watendaji wa wizara hiyo.
“Baada ya mkutano wa Bunge kumalizika, tutakwenda
kukaa na kuamua utaratibu tutakaotumia lakini sasa sina majibu,” alisema
na kuongeza kuwa baada ya wiki mbili atakuwa katika nafasi ya kusema
utaratibu utakaotumika kupanga matokeo hayo.
Hivi karibuni Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii,
katika taarifa yake ya utekelezaji wa shughuli zake katika kipindi cha
Machi hadi Desemba 2013, iliitaka Serikali kusitisha utaratibu mpya wa
upangaji wa matokeo ya mitihani.
Mabadiliko hayo, daraja ziro ambalo kwa muundo wa
zamani lilikuwa na alama 34-35 sasa litakuwa daraja la tano likiwa na
alama 48-49.
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi,
Profesa Sifuni Mchome alikaririwa na vyombo vya habari akisema muundo
huo mpya utatumika kwa mzunguko katika kipindi cha miaka minne.
Daraja la kwanza halijaathiriwa na muundo mpya,
kwani alama zake zimebaki pale pale ambazo ni 7-17. Daraja la pili alama
za muundo wa zamani zilikuwa 18-21 na sasa ni 18-24. Alama za daraja la
tatu zilikuwa 22-25 na chini ya muundo mpya zitakuwa 25-31, wakati
daraja la nne alama zimebadilika.
إرسال تعليق