Christian Bella kuachia wimbo wa R&B 'Utamtaka', sikiliza hapa akiimba kionjo cha wimbo huo

Mwimbaji wa muziki wa dansi kutoka Congo, Christian Bella amepanga kuachia wimbo wa mahadhi ya R&B hivi karibuni ambao ameuita ‘Utamtaka’.
 “Kuna R&B moja sasa natoa ya kwangu, naimba sasa R&B na nimeiandika mimi…utaisikia hiyo mwanangu.” Christian Bella ameiambia tovuti ya Times Fm.
“Nimeshatengeneza beat nadhani mpaka next week naiimba, ntaiweka kwenye albam yangu ntakuwa na mastyle tofauti tofauti naenda kuingiza sauti next week. Nimefanya kwa C9.             Ukiwa msanii lazima uonje style tofauti tofauti, lazima uoneshe ubunifu kwamba unaweza kufanya style zote.
“Ukisikiliza albam yangu ya Don’t Panic nilijaribu kufanya RnB fulani niliimba Africa. Ilikuwa kama RnB lakini, niliimba Africa Stand up na nilirap pia ndani. Mimi kila siku najaribu kufanya kitu ambacho sio utaarabu wangu ambao naimba. Naangalia pia beat nyingine pia nafanya nikiwa na albam watu wanasikiliza rhumba, mtu akisikiliza RnB mtu anaependa RnB anajikuta. Napiga ngoma msanii wa hip hop, unashirikisha msanii wa bongo flava”.  
Christian Bella hivi ambaye alikuwa anafanya kazi na bendi ya Akudo Impact, hivi sasa anafanya kazi na bendi ya Malaika.
Msikilize hapa akieleza na kutoa kionjo cha wimbo huo.

Post a Comment

أحدث أقدم