Niiteni MSODOKI msiniite YOUNG KILLER, Sababu hizi hapa

yong killerRapper wa ‘Mrs Superstar’ kutoka jiji la Miamba mwanza anataka kuanzia sasa aitwe MSODOKI na sio Young Killer tena kutokana na sababu moja kubwa.
Inawezekana umeshamskia sana Young Killer akitaja MSODOKI katika nyimbo zake, na pia analitumia katika mitandao ya kijamii, rapper huyo ameelezea lilipotoka jina hilo na sababu kubwa ya kutaka aitwe Msodoki badala ya Young Killer.
“Msodoki ni jina la familia yangu, familia yangu ndio inaitwa Msodoki, pia kipindi naanza kuitwa Young Killer nilikuwa under 18, saizi napenda sana kuitwa Msodoki kwasababu nishavuka sasa hivi nina miaka ishirini Ndio maana naliweka sana msodoki mbele”.Amesema Young Killer Msodoki kupitia XXL ya Clouds FM.
Msodoki leo ametambulisha single yake mpya ‘My Power’ iliyotengenezwa katika studio ya Classic Sound.

Post a Comment

أحدث أقدم